October 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kufukuzwa Membe: Fikra za Zitto, Lema

Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalando

Spread the love

HATUA ya Bernard Membe kufukuzwa uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), imeibua mjadala mitandaoni. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, amehusisha kufukuzwa kwa Membe, aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na dhamira yake (Membe), kutaka kugombea urais kupitia chama hicho kwenye uchaguzi mkuu wa 2020.

“Chama kikongwe kimetekwa na mtu mmoja. Mwanachama kaonesha nia tu ya kugombea urais ndani ya chama, kafukuzwa uanachama,” Zitto ameandika kupitiaukurasa wake wa twitter leo tarehe 28 Februari 2020 na kuongeza:  

“Bernard Kamilius Membe wamekutua mzigo hawa. Simamia unachokiamini na historia itakuweka unapostahili- kwamba ulikataa udikteta ndani na nje ya chama chako.”

Godbless Lema, Mbunge wa Arusha Mjini ameeleza, kwamba Membe ana bahati kubwa kwa kuondolewa dhambi (kufukuzwa CCM).

Kwenye ukursa wake wa twitter leo Lema ameandika “Bernard Kamilius Membe una bahati kubwa, kwani kufukuzwa CCM ni sawa na kuondolewa dhambi.

“Kama una hasira za dhati juu ya uonevu unao endelea pamoja na shida zinazo endelea nchini, sasa una nafasi nzuri ya kupigania utu kwa nguvu na ufasaha zaidi. Karibuni kazini.”

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, imemfukuza uanachama leo kwa madai ya utovu wa nidhamu. Hata hivyo, Membe ameeleza kwamba atazungumza kuhusu hatua hiyo.

error: Content is protected !!