Saturday , 25 March 2023
Home Kitengo Michezo Kufuatia kifo cha Magufuli, TFF yasimamisha michezo kwa wiki mbili.
Michezo

Kufuatia kifo cha Magufuli, TFF yasimamisha michezo kwa wiki mbili.

Clifford Ndimbo, Msemaji wa TFF
Spread the love

 

SHIRIKISHO la mpira wa Miguu Tanzania limesimamisha michezo yote kwa muda wa wiki mbili kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli kilichotokea jana kwenye hospitali ya Mzena iliyopo jijini Dar es Salaam. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam …  (endelea).

Kifo cha Rais Magufuli kilitangazwa jana tarehe 17 Machi 2021, na makamu ra Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu na kutangaza siku 14 za maombolezo.

Katika Taarifa iliyotolewa na idara ya Habari na mawasiliano ya TFF imeeleza kuwa, shirikisho hilo limesimamisha mechi zake zote ili kuungana na watanzania wote kuomboleza msiba wa Rais Magufuli.

Wakati huo huo TFF imefuta mchezo wa kiamataifa wa kirafiki kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya timu ya Taifa ya Kenya (Harambee Stars) uliopangwa kuchezwa leo jijini Nairobi nchini Kenya.

Aidha TFF imeeleza kuwa Taifa Stars itaendelea kusalia kenya kwa ajili ya maandalizi ya mchezo ujao wa kufuzu kombe la mataifa Afrika dhidi ya Equatorial Guinea na baadae kurejea nchini kuwakabili Timu ya Taifa ya Libya, tarehe 30 Machi, 2021.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Yanga: Fedha za Rais Samia zinaleta ari kubwa

Spread the loveUONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema fedha zinazotolewa na Rais...

Michezo

Simba Sc. yamvulia kofia Rais Samia, yamuahidi makubwa dhidi ya Horoya

Spread the loveWAKATI timu ya Simba ikiibuka na ushindi wa bao 3-0...

Michezo

Taasisi ya TKO na TFF yawapiga msasa makocha wa kike 54

Spread the love WAKATI Soka la wasichana likichipua kwa kasi Taasisi ya...

Michezo

Kimwanga CUP yazidi kutimua vumbi

Spread the loveMASHINDANO ya mpira wa miguu ya Kimwanga CUP ya kuwania...

error: Content is protected !!