KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Emmanuel Amunike, ametangaza kikosi cha wachezaji 32 watakaondoka leo kwenda Misri kwa ajiri ya kuweka kambi ya wiki mbili, kujiandaa na michuano ya kombe la mataifa Africa (AFCON) 2019, yatakayo fanyika nchini humo kuanzia tarehe 21 Juni, mwaka huu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea).
Kwenye kikosi chake, kocha huyo amewaacha wachezaji saba akiwemo nahodha wa klabu ya Yanga, Ibrahim Ajibu na kiungo mkabaji wa klabu ya Simba, Jonas Mkude ambao walikuwa kwenye kikosi hicho hapo awali, kilichokuwa na na jumla ya wachezaji 39.
Amunike ameeleza kuwaacha wachezaji hao kwa kutokuwa na nidhamu pia kutojituma mazoezini. Wengine walioachwa ni Ally Ally (KMC), Kennedy Juma (Singida United), Ayoub Lyanga (Coastal Union), Kassim Khamis (Kagera Sugar) na Shomari Kapombe (Simba SC).
Wachezaji ambao wataambatana na timu hiyo kwenda Misri ni Aishi Manula (Simba SC), Metacha Mnata (Mbao FC), Suleiman Salula (Malindi FC), Aron Kalambo (Tz Prisons), Claryo Boniphace (U20).
Pia Hassan Kessy (Nkana FC), Vicent Philipo (Mbao FC), Gadiel Michael (Yanga SC), Abdi Banda (Baroka FC), Ally Mtoni (Lipuli FC), Mohamed Hussein (Simba SC), Agrey Moris (Azam FC), Kelvin Yondan (Yanga), Erasto Nyoni (Simba SC), David Mwantika (Azam FC).
Wamo Feisal Salum (Yanga SC), Himid Mao (Petrojet), Mudathir Yahya (Azam FC), Frank Domayo (Azam FC), Fred Tangalu (Lipuli FC), Yahya Zayd (Ismailia), Miraji Athuman (Lipuli FC), Farid Musa (Tenerife), Shiza Kichuya (ENPPI), Saimon Msuva (Difaa El Jadidi).
wengine ni Shaban Chilunda (Tenerife), Rashid Mandawa (BDF), Mbwana Samatta (KRC Genk), Thomas Ulimwengu (JS Saoura), John Bocco – (Simba SC), Kelvin John (U17) na Adi Yusuph (Blackpool).
Tanzania ambayo imepangwa kwenye kundi C kwenye michuano hiyo, inatarajia kutupa karata yake ya kwanza dhidi ya Senegal tarehe 23 Juni 2019 na baadaye dhidi ya Kenya kisha kumaliza na Algeria.
Leave a comment