April 11, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kuchomwa bendera; CUF yatinga kortini

Halifa Suleiman Halifa, Katibu Mkuu wa CUF akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam

Spread the love

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimefungua shauri mahakamani visiwani Zanzibar kushitaki watu wanaodaiwa kuchoma bendera zake pia kupaka rangi ya bendera ya Chama cha ACT-Wazalendo katika majengo yao. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Halifa Suleiman Halifa, Katibu Mkuu wa CUF akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo tarehe 26 Machi 2019 amesema, kesi hiyo imefunguliwa katika Mahakama Kuu ya Vuga visiwani Zanzibar.

Kiongozi huyo wa CUF ameeleza kuwa, wamefungua kesi hiyo baada ya kukusanya ushahidi wa matukio hiyo, ikiwemo kupata majina ya wanayodaiwa kuhusika kuchoma bendera za CUF kubadili rangi za ofisi ya chama hicho na kupaka rangi na nembo za chama cha ACT-Wazalendo.

“Baada ya hapo tukakubaliana tukusanye ushahidi, yote yaliyofanyika, majina ya waliotumika kufuta rangi za chama chetu, waliopachua bendera zetu na kuchoma moto, ushahidi uhuo tumeukamilisha na kufungua kesi katika Mahakama Kuu ya Vuga,” amesema na kuongeza;

“Sasa sheria itachukua mkondo wake, sasa wasishangae moto wao.  Wanasema ShushaTangaPandishaTanga, itamalizikia matanga.

“Kwa tabia hii ya kudhani mtu ni chama ni hatari chama ni taasisi, walipopachua ofisi ya Kilimahewa watu waliwaambia wasipachue, Salim Bimani alisema hilo ni agizo la Maalim Seif.”

error: Content is protected !!