Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kucha na kope bandia marufuku bungeni
Habari za SiasaTangulizi

Kucha na kope bandia marufuku bungeni

Spread the love
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Job Ndugai, amepiga marufuku wabunge wanawake kuingia bungeni wakiwa wamebandika kucha na kope za bandia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

“Kwa mamlaka niliyopewa, napiga marufuku wabunge waliobandika kucha za bandia na kope za bandia kwamba ni marufuku na hilo la kujipodoa bado najadiliana na wataalam wangu,” amesema Spika.

Spika Ndugai alitoa kauli hiyo leo bungeni muda mfupi baada ya Naibu Waziri wa afya, Dk Faustin Ndugulile kutoa majibu ya madhara makubwa wanayopata wanawake wanaotumia kucha na kope za bandia.

Naibu Waziri alisema takribani wagonjwa 700 hupokelewa kwa mwaka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wakiwa na matatizo ya ngozi yatokanayo na kumeza vidonge vinavyobadili sura pamoja na vipodozi vyenye kemikali na kuwa watu hao wapo kwenye hatari ya kupata magonjwa ya saratani na ya ngozi.

Katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Fatuma Toufiq alihoji ni wanawake wangapi wameathirika macho kutokana na matumizi ya kope bandia.

Naibu Waziri alisema kucha na kope za kubandika si vipodozi kwa mujibu wa sheria ya chakula, dawa na vipodozi sura ya 219 inayosimamiwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA).

“Kwa mujibu wa sheria hiyo, kipodozi ni kitu chochote kinachotumika kwenye mwili au sehemu ya mwili,” alisema Dk Ndugulile.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!