Friday , 9 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kubenea: Wabunge CCM wanajali matumbo, chama chao
Habari za Siasa

Kubenea: Wabunge CCM wanajali matumbo, chama chao

Saed Kubenea
Spread the love

SAED Kubenea, mgombea ubunge wa Jimbo la Kinondoni kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, amesema Abbas Tarimba, mgombea ubunge katika jimbo hilo kupitia CCM, ana tabia zile zile walizonazo wabunge wanaotokana na chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Amesema, tabia ya wabunge wanaotokana na chama hicho, ni kutumikia matumbo yao na chama chao badala ya wananchi waliowaweka madarakani.

“Kila mbunge wa CCM anapokwenda bungeni, anakuwa na mambo mawili, kwanza chama chake na tumbo lake, kwa hiyo Abbas Tarimba anakwenda kutetea CCM na kutetea mchezo wake wa kamari.” amesema Kubenea

“Nimekuwa mbunge miaka mitano, nimekuwa mwandishi wa bunge kwa zaidi ya miaka 17, ninafahamu wafanyabiashara wote wa kamari na casino wanavyoteka kamati ya bajeti.”

Kubenea ambaye aliyekuwa mbunge wa Ubungo kupitia Chadema (2015 – 2020), ametoa kauli hiyo tarehe 30 Septemba 2020 katika mkutano wa kampeni uliofanyika Magomeni Mzimuni, jijini humo.

Amesema, Kinondoni inamuhitaji mtu mwenye muda wa kutosha kuwatumikia wananchi na aliyejitoa kwa dhati ambaye ni yeye.

Kubenea amesema, Tarimba ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania inayojihusisha na michezo ya bahati nasibu, hawezi kuwa na muda wa kujua shida za wa nanchi na kuzitatua.

“Wakati wa Bunge, miswada inayohusu michezo ya kamari na michezo ya bahati na nasibu, serikali inachukua mapato ya kodi nyingi, kina Abbas Tarimba wanakuja bungeni kutaka ifanyiwe marekebisho,” alisema

Kubenea alitumia fursa hiyo kuelezea mchakato wa kupata mgombea ubunge wa Kinondoni kupitia CCM jinsi chama hicho kilivyoshindwa kushughulikia malalamiko ya wale walioshiri.

“Chagueni mbunge atakayekwenda bungeni kupeleka kitu chenu, msichague mbunge ambaye hatokuwa na muda nanyi bali kwenda kutetea biashara yake na chama chake.

“Hata leo (jana) kulikuwa na msiba hapa, Tarimba ameishia pale nyumbani makaburini hakwenda, ameswalia pale, amekula pilau kisha huyo, hajapata ubunge hajakwenda kuzika, akipata ubunge je,” alihoji Kubenea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lussu: Mkataba wa DP bandarini si wa miaka 100

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema hakuna ukweli wowote...

Habari za SiasaTangulizi

Maulid Mtulia: Kutoka ubunge hadi U-DAS

Spread the love ALIYEKUWA mbunge wa Kinondoni, kupitia vyama vya The Civil...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

error: Content is protected !!