February 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kubenea: Tutashinda na tutatangazwa washindi

Spread the love

MBUNGE wa Chadema jimbo la Ubungo, Saed Kubenea amesema, ni lazima chama chake kiibuke kidedea kwenye kinyang’anyiro cha ubunge jimboni Kinondoni. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kigogo leo Jumanne, Kubenea amesema, ushindi kwa Chadema unatokana na makosa ya mshindani wao katika kuteuwa mgombea.

“Ni lazima tutashinda uchaguzi huu. Ni kwa sababu, tuna mgombea mzuri ukilinganisha na CCM na kwamba chama hicho tawala kimedharau wananchi,” ameeleza Kubenea.

Amesema, “kuna wanaopita mitaani na kusema, hata tukishinda hatutangazwa. Nataka kuwaambia, hawatujui. Nataka kuwaambia tutashinda na tutangazwa.”

Uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Kinondoni unafanyika kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa mbunge wake, Maulid Said Mtulia, aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Wananchi (CUF).

Kubenea ndiye meneja kampeni wa mgombea ubunge wa Chadema katika jimbo la Kinondoni, Salum Mwalimu.

error: Content is protected !!