Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kubenea: Tume ifute uchaguzi Kinondoni
Habari za Siasa

Kubenea: Tume ifute uchaguzi Kinondoni

Spread the love

MGOMBEA Ubunge wa Kinondoni kupitia ACT-Wazalendo, Saed Kubenea ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kufuta uchaguzi katika jimbo hilo kwa madai ya kuharibiwa kwa shughuli hiyo mara baada ya kuzuiliwa kwa mawakala wao kuingia kwenye vituo vya kupigia kura mapema. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kubenea amesema hayo mapema hii leo Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 alipozungumza na waandishi wa habari huku akiwa ameambatana na mgombea wa Ubunge jimbo hilo wa NCCR Mageuzi Mustapha Muro.

Mgombea huyo amesema, kwa sasa kinachoendelea sio uchaguzi bali ni uchafuzi kwa kuwa kumekuwepo na viashilia vingi vya kutaka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushinda uchaguzi huo kwa njia ambazo si zahaki.

“Tunaomba tume ifute uchaguzi huu kwa jimbo la kinondoni ili kutenda haki na zoezi hilo liitishwe upya kwa kusimamiwa na tume yenyewe kwa kuwa mpaka sasa hivi kura zaidi  ya 10000 zimeingizwa kwenye masanduku ambazo sio halali kuanzia majira yaa saa 1 mpaka saa 3 asubuji” amesema Kubenea

Madai hayo ya mgombea huyo yamekuja mara baada ya kudai msimamizi wa uchguzi katika jimbo hilo amevuruga uchaguzi huo kwa makusudi na kudhamilia kwa kuwa walikataa kuingiza mawakala wao mapema katika vituo na kufanya kura nyingi kupigwa kabla ya vituo kufunguliwa.

“Kituo cha shule ya msingi Mwenge, mawakala wetu walifika saa 11 alfajili walikuta geti limefungwa na mlinzi akasema muda wa kufungua kituo bado, lakini walivyofika ndani mara baada ya muda kidogo likaja gari aina ya Toyota Harrier ikiwa na wapiga kura aliwaingiza ndani na kupiga kura nyingi walivyotaka bila kuwepo mawakala,” amesema Kubenea.

Kubenea amesema, kwa kusema kwenye baadhi ya vituo vingine mawakala wao walizuiliwa kuingia licha ya kufanikiwa kuwasiliana na mkurugenzi wa tume hiyo na kumueleza hali halisi ya zoezi hilo linavyoendelea.

Aidha mgombea huyo amesema, tayari ameshaandika  barua tume kumlalamikia msimazi wa uchaguzi jimbo la kinondoni Aron Kagurumjuli huku nakala ya barua hiyo akipeleka polisi na nakala moja kumkabidhi yeye mwenyewe.

Zoezi la wananchi kupiga kura limeanza mapema hii leo kuanzia majira ya saa 1 kamili Asubuhi ambapo litadumu mpaka saa 10 kamili jioni kwa mujibu wa sharia ya tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Kwa upande wake, Muro amesema, kitendo cha mawakala wao kuzuiwa kuingia mapema vituoni imewafanya kukosa imani ya kile kilichokuwa kikiendelea kwenye vituo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!