August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kubenea, Manase wakana kumshambulia Mmbando

Spread the love

MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea na Manase Mjema, Diwani wa Kimanga wamekana kumshambulia Terresia Mmbando, Katiba Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, anaandika Faki Sosi.

Watuhumiwa hao wamekana mashitaka yao wakati wakisomewa leo asubuhi katika Mahakama ya Mkazi Kisutu baada ya kutuhumiwa kumshambulia Mmbando wakati wa mkutano wa uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam tarehe 27 Februari 2016.

Kubenea amabye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers anatajwa kuwa ni mtuhumiwa namba sita ambapo Manase akiwa mtuhumiwa namba nne.

Mmbando alikuwa mwenyekiti wa mkutano wa kumchagua Meya wa Jiji la Dar es Salaam uliofanyika kwenye Ukumbu wa Kareem Jee na baadaye kuahirishwa hatua ambayo iliibua malumbano.

Mbele ya Cyprian Mheka, Hakimi Mkazi Kisutu washitakiwa hao walikana kosa hilo ambapo hakimu alighairisha kesi hiyo mpaka tarehe 16 Machi mwaka huu.

Hata hivyo, Hakimu Mkeha aliwataka watuhumiwa hao kujidhamini wenyewe kwa dhamana ya Sh. 2,000,000 sharti ambalo walilitekeleza.

Jana asubuhi kwenye mahakama hiyo Kubenea akihudhuria kesi yake dhidi ya Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, alikamatwa na Jeshi la Polisi na kuwekwa chini ya ulinzi.

Kubenea na Manase wameunganishwa kwenye kesi hiyo ambapo watuhumiwa waliofikishwa mahakamni awali Halima Mdee, Mbunge wa Kawe; Mwita Waitara, Mbunge wa Ukonga na madiwani wawili jumla yao ikiwa ni watuhumiwa sita.

error: Content is protected !!