July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kubenea kutunukiwa Tuzo

Saed Kubenea, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited

Spread the love
MKURUGENZI Mtendaji wa kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited, Saed Kubenea, leo anatarajiwa kukabidhiwa tunzo ya ushujaa uliotukuka kutokana na mchango wake kwa taifa. Anaandika Pendo Omary … (endelea).
 
Taarifa kutoka jijini Dar es Salaam na ambazo zimethibitishwa Kubenea mwenyewe zinasema, Tuzo hiyo itatolewa na shirika moja lisilo la kiserikali, liitwalo, “Dream Success Enterprise (DSE)” la jijini Dar es Salaam.
 
Mbali na Kubenea, wengine wanatarajiwa kutunukiwa Tuzo hizo, ni Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR- Mageuzi), David Kafulila na mtangazaji wa zamani wa BBC, Vicky Mtetema.
 
Kubenea ambaye pia ni mhariri mtendaji wa magazeti ya MwanaHALISI, MSETO na gazeti la mtandao – MwanaHALISI Online, atakabidhiwa Tuzo ya Uwazi na Ukweli.
 
Naye Kafulila atakabidhiwa Tuzo ya Maono Mapevu; huku Vicky akikabidhiwa Tuzo ya Ubunifu.
 
“Napenda kuchukua fursa hii kukupongeza kwa kutunukiwa Tuzo hii adhimu. Natoa shukurani zangu za dhati kwa mchango wako wa hali na mali katika taifa letu. Umefaanya kazi kubwa isiyopimika,” anaeleza Mtetema katika taarifa yake kwa Kubenea.
Anasema, “…umefanya kazi kubwa kwa manufaa ya wengi licha ya wachache kukupinga kwa ubinafsi wao na wakati mwingine kuhatarisha maisha yako.”
 
Mtetema anasema, Tuzo hiyi inadhihirisha jinsi gani mchango wa mwanahabari huyo mwenzake unavyowagusa watu wengi na unavyotambuliwa na watu wanaolitakia mema taifa hili.
 
“…usichoke kupigania haki kwa ajili ya wengi. Namuomba Mungu akulinde na aendelee kukubariki,” ameeleza Mtetema.
 
Taarifa zinasema, Tuzo hiyi iliyoanzishwa mwaka 2014 na kuzinduliwa tarehe 22 Desemba iliwahi kutolewa kwa aliyekuwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh.
error: Content is protected !!