January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kubenea kurejesha UDA kwa wananchi

Spread the love

MGOMBEA ubunge katika Jimbo la Ubungo, Dar es Salaam Said Kubenea, amesema Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) lililobinafsishwa kwa kuuzwa hisa zake kifisadi atalirejesha mikononi mwa wananchi. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Hata hivyo Kubenea ameahidi kutaja majina ya watu waliochota fedha za Escrow endapo atachaguliwa na wananchi wa Ubungo kuwa mwakilishi wa jimbo hilo bungeni.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kampeni zake kwenye viwanja vya Faru, Mabibo jijini Dar es Salaam Kubenea amesema, waraka wa serikali ulikataza uuzwaji wa hisa hizo lakini ushauri huo ulipuuzwa na Meya wa Jiji Dk. Didai Masabu ambaye alisimamia uuzwaje wa hisa hizo kifisadi.

Akinukuu barua iliyoandikwa 28 Februari 2011 Kubenea amesema, “nikichaguliwa nitahakikisha shirika la UDA linarudi mikononi mwa umilikiwa wa wananchi.”

Akizungumzia kuhusu sakata la Escrow Kubenea amesema, “Mkinichagua kuwa mbunge wenu na kwa kuwa nitakuwa na kinga ya bunge nitataja majina ya waliochukua fedha za Escrow katika benki ya Stanbic,” amesema Kubenea.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na baadhi ya viongozi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, Kubenea amesema baada ya kutumia kalamu yake kwa miaka 10 sasa anataka kuwawakilisha wakazi wa Ubunge bungeni Dodoma kama mbunge wao.

“Baada ya miaka 10 kutumia kalamu yangu kuwatetea Watanzania, sasa nataka kutumia mdomo wangu kuwatetea wananchi katika Bunge la Tanzania,” amesema Kubenea na kuongeza;

“Nataka kwenda bungeni kwa kuwa mamilioni ya Watanzania wananyanyaswa na CCM na hawana wa kuwasemea lakini pia nataka kumaliza kazi ambayo ameianza Mnyika (John Mnyika) ikiwa ni kusimamia ujenzi wa barabara, kuimarisha hospitali zetu zote, kuimarisha shule za Kata na elimu bure kwa Watanzania wote.”

Mgombea huyo amesema, anayafahamu matatizo ya wakazi wa Ubungo na kwamba kama anayaorodhesha basi yangechukua zaidi ya saa moja.

“Ninawahakikishia wakazi wa Ubungo, mkinichagua kuwa mbunge wenu nitakuwa mbunge bora na mtatembea kifua mbele kwamba, mmempata mbunge thabiti,” anasema.

Kuhusu utendaji kazi wa mgombea urasi wa CCM, Dk. John Magufuli, Kubenea amesema anamfahamu vizuri mgombea huyo, CCM na utendaji wa serikali na kwamba, si mbunifu.

Amekumbushia dhamira ya Magufuli ya kutaka kuvunja Makao Makuu ya Tanesco yaliyopo Barabara ya Morogoro, Ubungo ili kupitisha barabara badala ya kufikiria kujenga barabara za juu ili kuokoa mamilioni ya fedha yaliyotumika kujenga jengo hilo.

“Jengo la Makao Makuu ya Tanesco limegharimu mamilioni ya fedha za wananchi yeye anafikiria kulibomoa wakati angeweza kujenga barabara za juu kukabiliana na foleni, hafikirii huyo.” anasema Kubenea na kuongeza;

“Baada ya wabunge na Bodi ya Tanesco kupiga kelele, mradi wa kuvunja ukakwama.”

Hata hivyo ameeleza zilzojengwa na Magufuli hazidumu kwa muda mrefu na huharibi ndani ya miezi michache.

Akimzungumzia mgombea urais wa Chadema na anayeungwa mkono la UKAWA, Edward Lowassa, Kubenea amesema hoja zinazoletwa na CCM juu ya tuhumiwa za ufisadi wa Lowassa kuhusu Kampuni ya Kufua Umeme ya Richmond hazina msingi na zimepitwa na wakati.

“Nimeandika Richmond kwa zaidi ya miaka minane, ninayajua mengi. Kamati ya Bunge iliyoundwa ilikuwa na ripoti mbili, moja ya Mwakyembe (Dk. Harrison Mwakyembe) nyingine ya Sitta (Samuel Sitta). Mpaka leo ya Sita hajaitoa,” amesema.

Amesema, Mwakyembe katika ripoti yake alisema, kuna mambo waliyaficha na wangeyasema serikali ingeanguka huku akihoji ni mambo gani.

Ameongeza, “Waziri Mkuu alijiuzulu. Je, serikali ambayo Mwakyembe alisema ingeanguka, ni serikali gani?” amehoji?

Amesema, katika hatua zote za Richmond hakunahatua hata moja aliyoifanya Lowassa bila kumtaarifu bosi wake ambaye ni Rais Jakaya Kikwete.

error: Content is protected !!