January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kubenea kumshitaki Meneja wa Kituo cha Mabasi Ubungo

Spread the love

MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea, amesema atamshitaki Meneja wa Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani (UBT), Juma Idd, kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe, kutokana na kushindwa kutatua kero zilizoko katika kituo hicho. Anaandika Josephat Isango … (endelea).

Kubenea alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea kituoni hapo kuona utekelezaji wa makubaliano kati yake na Meneja huyo ya kumaliza kero za kituo hicho waliyoafikiana wiki iliyopita.

Alisema mambo waliyokubaliana na Meneja huyo ni pamoja na usafi katika eneo hilo ikiwamo kutengeneza mifumo ya kupitishia maji taka, kuzibua mitaro  iliyoziba,  kuondoa madampo ya uchafu, kusafisha maeneo mengine machafu katika eneo hilo pamoja na kero nyingine wanazozilalamikia wafanyabiashara.

“Wiki iliyopita nilitembelea kituoni hapa, pamoja na mambo mengine nilikagua hali ya usafi na kusikiliza kero za wananchi, tulizungumza na Meneja wa kituo tukakubaliana kwamba hizo kero zote atazifanyia kazi lakini nimerudi tena kuangalia hakuna kilichofanyika,” alisema Kubenea na Kuongeza:

“Nimefika ofisini kwa Meneja lakini hajaniruhusu niingie kumuona ili tuzungumze nifahamu ni tatizo gani ambalo limekwamisha kero hizi kutekelezwa, nimesimama sana mlangoni lakini hata waliokuwa nyuma yangu wameruhusiwa kuingia kumuona mimi nimeachwa, ninachosema ni kwamba hajanidharau mimi bali wananchi wa Ubungo.”

Aliongeza kuwa atafikisha kero hizo kwa bosi wake, na endapo naye atashindwa kuzifanyia kazi inavyostahili, ataziwasilisha katika baraza la Madiwani ambalo lina nguvu ya kuamua kumuondoa katika nafasi hiyo au laa pale linapoona hatekelezi majukumu yake ipasavyo.

error: Content is protected !!