July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kubenea: Kuhamisha stendi ya Ubungo ni Ufisadi

Spread the love

MBUNGE wa  Ubungo, Saed Kubenea, amesema anatarajia kupeleka hoja binafsi bungeni ili kuzuia kuhamishwa kituo cha mabasi yaendayo mikoani (UBT). Kwani kwa kuhamisha kituo hicho ni matumizi mabaya ya fedha za wananchi,  Anaandika Josephat Isango … (endelea)

Kubeana alitoa kauli hiyo alipofanya ziara katika jimbo  hilo, ikiwamo kuwashukuru wananchi kwa kumchagua, kukagua hali ya usafi katika masoko, ikiwamo stendi hiyo ya UBT  pamoja na kusikiliza kerombalimbali za wananchi.

Alisema ni vema stendi hiyo ikaendelea kuwapo katika eneo hilo,  kwa kuwa itasaidia katika kutengeneza biashara nzuri kutokana na kujengwa kwa mradi huo wa mabasi yaendayo haraka(Dart).
“Uwepo wa daraja la mabasi yaendayo kwa kasi hapa eneo la Ubungo ni ushahidi kuwa stendi hii ilikuwa inahitajika hapa, hatuwezi kujenga miundo mbinu yote hii kwa pesa za wananchi halafu tukahamisha, hayo ni matumizi mabaya ya pesa za wananchi” alisema Kubenea.

Kadhalika, Kubenea alikagua hali ya usafi na katika  eneo hilo la ubungo  ikiwa ni pamoja na kukagua katika vyoo , huku akionekana kukerwa na uchafu katika vyoo hivyo.
Kubenea ambaye  ni Mbunge wa pili kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kushika jimbo hilo,  baada ya kushikiliwa na John Mnyika kwa miaka mitano,  ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Kibamba, alisema atafanya kazi kufa na kupona ili kuhakikisha kero zote zinatatuliwa.
Aidha, Kubenea ameanza kutekeleza ahadi zake alizoahidi katika kipindi cha kampeni kwa kuanza kuchimba kisima cha maji katika soko la  Mabibo  kwa garama zake mwenyewe na kuagiza uongozi wa soko hilo kuongea  na mawakala wanaohusika na uchimbaji wa visima ili kazi hiyo ianze mara moja.

Mwenyekiti wa wafanyabiasha wa soko la mabibo, Yusuph Kirema alimshukuru Kubenea kwa kuwtembelea na kujua kero mbalimbali, hivyo watampa ushirikiano kwa maendeleo ya wananchi kwenye eneo  hilo.

error: Content is protected !!