April 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kubenea kufuta machozi walimu Shule za Msingi Mburahati, Karume

Spread the love

SAED Kubena, Mbunge wa Jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam ameahidi kukarabati ofisi za walimu ili kutatua kero zao za kufanyia kazi nje ya ofisi. Anaripoti Mwandishi wetu … (endelea).

Akiwa kwenye ziara yake jimboni humo leo tarehe 8 Machi 2019 amesema, atasaidia kutoa kiasi cha fedha kwa ajiri ya matengenezo ya ofisi hizo za walimu katika Shule ya Msingi Mburahati na Karume atalipatia ufumbuzi.

Katika Shule ya Msingi Karume Kubenea akiwa na watendaji wengine, alikutana na changamoto ya walimu kufanya kazi nje ya ofisi kutokana na jengo kuwa chakavu pia kutishia usalama wao.

Baada ya kukutana na changamoto hiyo Kubenea amesema, hivi karibuni atatoa kiasi kidogo cha fedha kwa ajili ya kufanya marekebisho ili walimu waweze kufanya kazi katika mazingira mazuri.

“Tutajitahidi kwa kadri tutakavyoweza ingawa gharama ni kubwa sana, kwa hiyo tutasaidiana,” amesema mbunge huyo.

Katika Shule ya Msingi Mburahati  ujenzi wa ofisi za walimu umeanza kufanyika huku akiahidi kutenga kiasi cha fedha ili kukamilisha ikiwa ni pamoja na vyoo vya wanafunzi vitavyogharimu Sh. 32 milioni.

Pia Kubenea alitembelea eneo la Mburahati Kata ya Makurumla nakujionea adha ya kivuko hasa wakati wa mvua, na wananchi wanashindwa kupita kutokana na kujaa maji.

Diwani wa kata hiyo Omary Thabiti amemwomba Kubenea kutengewa fedha ili kutatua kero hiyo ambayo wananchi wameizungumzia.

“Tutengeeni fedha sisi watu wa Kata ya Makurumla. Mitaa hii miwili tutazungumza na kuangalia eneo gani litafaa kuweka kivuko,” amesema.

Kubenea amefungua mwaka kwa kutembelea maeneo yote ya jimbo hilo ili kuhakikisha miradi ya maendeleo ya mfuko wa jimbo inatekelezwa.

Tazama video kamili hapo chini

error: Content is protected !!