January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kubenea kuboresha kituo cha Afya Palestina

Spread the love

MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema) amewahurumia akina mama wanaolazwa kwenye wodi ya wazazi ya hospitali ya Sinza Palestina baada ya kufika kujionea hali ya hospitali hiyo na kubaini uwepo wa changamoto mbalimbali ikiwemo ufinyu wa majengo hivyo kuahidi kuanza utaratibu wa kuboresha majengo hayo. Anaandika Josephat Isango … (endelea).

Akiwa ameambatana na waandishi wa habari, Kubenea amesema atahakikisha anapambana Bungeni na kwenye baraza la madiwani kuhakikisha hospitali hiyo inapanuliwa kwa ujenzi wa majengo ya kwenda juu.

Amesema hali ya kina mama wajawazito aliowakuta wamelala chini haijamridhisha ukizingatia kwamba hali wanayopitia wanapaswa kupumzika sehemu nzuri kutokana na uchovu wanaoupata baada ya kujifungua.

Awali akitoa taarifa kwa Mbunge huyo Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Hugolin Mselle, amesema pamoja na hospitali hiyo kupandiswa hadhi na kuwa ya Wilaya bado bajeti wanayoipata ni ile ambayo walikuwa bado ni kituo cha afya.

Kutokana na hilo amesema wamejikuta wakishindwa kuiendeleza hospitali hiyo ikiwemo kuboresha miundombinu ya upatikanaji wa huduma.

Kuhusu suala la wajawazito, amesema wamekuwa wakipokea idadi kubwa ukilinganisha na nafasi walioyanayo jambo linalowafanya kuhamishia wengine katika hospitali ya Mwananyamala hasa katika kipindi cha wamama wengi wanapojifungua ambacho ni kuanzia Januari hadi Agosti.

“Hospitali yetu ina uwezo wa kusaidia akina mama angalau kumi kwa siku kujifungua lakini tumekuwa tukipata watu zaidi ya 40 kwa siku hali inayoleta ugumu kwenye utendaji wa kazi” amesema Dk Msele

error: Content is protected !!