Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kubenea kuanzisha benki, kiwanda cha taka Kinondoni
Habari za Siasa

Kubenea kuanzisha benki, kiwanda cha taka Kinondoni

Spread the love

SAED Kubenea, Mgombea Ubunge wa Kinondoni kupitia ACT-Wazalendo amesema, ana mpango wa kuanzisha benki kwa ajili ya wananchi wa jimbo hilo. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea).

Kubenea ameyasema hayo jana Jumapili tarehe 11 Oktoba 2020 katika mwendelezo wa kampeni zake ndani ya jimbo hilo ambapo alifanya mikutano ya wazi Mwananyamala na Magomeni.

“Tunataka kuboresha maisha ya Watanzania wenzetu wa manispaa ya Kinondoni hasa wafanyabiashara ndogo ndogo na bodaboda kwa kuanzisha benki ya wananchi wa kinondoni itakayofanya kazi kama ilivyokuwa benki ya Dar es Salaam (DCB)” amesema Kubenea.

Aidha, amesema, benki hiyo itatoa mikopo kwa wafanyabiashara hao ambapo itawawezesha kuendeleza biashara zao.

“Tunayo rekodi na haiwezi kutiliwa mashaka ya uaminifu na uadilifu wetu, angalieni watu wanaofanana na nyinyi ili waweze kuwatetea” amesema.

Amesema, kwa miaka mingi amefanya kazi ya utetezi kupitia vyombo vya habari na pia amefanya hivyo hivyo akiwa mbunge wa Ubungo pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali hivyo anataka kurudi bungeni kuimarisha kazi hiyo ili serikali isikilize wananchi wake na kutatua matatizo yao.

“Nitumeni mimi nipo tayari kuwatunikia, sijawahi kushindwa kazi na nina rekodi ya uaminifu katika utumishi wangu, nipelekeni. Bungeni nikafanye kazi hiyo.”

Sera nyingine ambazo Kubenea amewaeleza wananchi wa Kinondoni ni pamoja na kuhakikisha kila mtu aliyetimiza miaka 60 apate matibabu bure hospitali pamoja na kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa na bima ya afya.

Jambo lingine ni kuondoa tozo za kuhifadhi miili ya marehemu waliofia katika hospitali ya serikali, kutatua kero ya mafuriko kwa kuujenga upya mto Msimbazi na kuufanya juwa eneo la kivutio cha utalii.

Kubenea amesema, akiwa Mbunge wa Kinondoni atahakikisha Dar es Salaam suala la taka linakomeshwa kwa kujenga kiwanda cha kuzalisha mbolea zinazotokana na taka ngumu.

Mgombea Ubunge wa Kinondoni kupitia ACT-Wazalendo, Saed Kubenea akinunua na kula samaki mara bada ya kumaliza mkutano wa kampeni eneo la Magomeni Morocco jana jioni Jumapili.

Amesema, walipanga kujenga kiwanda hicho Kinondoni kati ya mwaka 2015-2020 wakati halmashauri hiyo ikiongozwa na upinzani, lakini ilipogawanywa na kutoka mbili ya Ubungo na Kinondoni na Kinondoni kuanza kuongozwa na meya wa CCM, mpango huo ulikufa uliokuwa utekelezwe na wadau wa maendeleo.

Kubenea amesema, akiwa mbunge, watakwenda kuendeleza mpango huo waliouanzisha ili kijengwe kwani kitatoa pia ajira na kuweka jiji safi akisema “wao wanawaita mabeberu, sisi tunawaita wadau wa maendeleo

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!