March 7, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kubenea, Komu wapewa onyo kali, wawekwa chini ya uangalizi

Spread the love

KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewapa onyo kali wabunge wake Saed Kubenea wa Ubungo na Anthony Komu wa Moshi Vijijini kufuatia kuwatia hatiani juu ya kuunda njama ovu dhidi ya Mwenyekiti Freeman Mbowe na Meya wa Ubungo, Boniface Jacob. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika amesema Kamati Kuu imewatia hatiani wabunge hao baada ya kuwatia mbele ya kamati hiyo kujieleza na wote wamekiri kuwa sauti iliyosambaa ni yao wameomba radhi.

Mnyika amesema baada ya wabunge hao kukiri na kuomba radhi, kamati imefanya maamuzi juu ya makosa yao, kwanza kuwapa onyo kali, pili waandike barua ya kuomba radhi kwa chama.

Pia Mnyika amesema kamati kuu ikafikia uamuzi wa kuwaweka kwenye uangalizi kwa miezi 12, ikiwa oamoja na kuwavua nafasi zao zote za uongozi ndani ya chama na kubaki na ubunge.

Naibu Katibu amesema adhabu ya mwisho kwa wabunge hao ni kutoka hadharani kuomba radhi kwa makosa waliyofanya dhidi ya viongozi wa chama hicho.

error: Content is protected !!