November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kubenea, Komu waanza kuhojiwa na Kamati Kuu Chadema

Anthony Komu Mbunge wa Moshi Vijijini na Saed Kubenea wa Ubungo

Spread the love

WABUNGE Saed  Kubenea (Ubungo) na Anthony Komu (Moshi Vijijini) wameanza kuhojiwa na Kamati Kuu ya Chadema katika kikao cha kamati hiyo kinachoendelea leo Jumatano Oktoba 17, 2018 katika ukumbi wa Ledger Plaza katika Hoteli ya Bahari Beach. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kikao hicho pamoja na ajenda nyingine lakini pia kimekutana kuwajadili wabunge hao wawili baada ya kudaiwa kupanga mpango hasi dhidi ya Meya wa Ubungo, Boniface Jacob kupitia kile kinachodaiwa sauti iliyotengeneza ya mpango huo.

Kubenea na Komu katika siku za hivi karibuni wamezua mjadala ndani na nje ya chama hicho baada ya kuvuja kwa sauti hiyo ambayo inadaiwa ni mazungumzo kati ya wabunge hao.

Wabunge hao waliwasili ukumbi hao majira ya saa 8:01 mchana ambapo baada ya kupewa maelezo, Komu ndiyo alikuwa wa kwanza kuingia kuhojiwa mbele ya kamati hiyo huku Kubenea akisubiri muda wake kuitwa.

error: Content is protected !!