June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kubenea: Ili tufanikiwe tuweke pembeni itikadi zetu

Spread the love

MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea amefanya ziara katika Kata ya Makurumla iliyoko jimboni kwake na kutembelea masokoni, Zahanati na shuleni. Anaandika Josephat Isango(endelea).

Katika ziara hiyo aliwaomba viongozi wa serikali za mitaa, wajumbe na mtendaji wa Kata hiyo, kufanya kazi ya kutumikia wananchi kwa bidii na kuweka itikadi za vyama vyao pembeni.

Kubenea aliwaambia wananchi wa Makurumla kuwa ili wafanikiwe katika kipindi hicho cha miaka mitano ambacho wameaminiwa na wannachi wanahitaji kufanya kazi  kwa ushirikiano pasipo mikwaruzano.

Kadhalika, Kubenea alikerwa na kuwapo kwa mrundikano wa taka zilizopo katika soko la sisi kwa sisi katika Kata hiyo ambazo zilizolewa  katika siku ya Uhuru na kushindwa kuondolewa.

Aliahidi kurejea hapo na Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni, kutafuta ufumbuzi juu ya mitaro iliyoziba ili kuweka soko hilo katika usafi.

Aidha akiwa Zahanati ya Makurumla, Kubenea alielezwa upungufu wa dawa, kukosekana kwa maji safi yasiyo ya chumvi na gari la kubebea wagonjwa.

Akijibu masuala hayo, Kubenea aliuhakikishia uongozi wa Zahanati hiyo kufuatilia changamoto hizo kwani zipo chini ya uwezo wa Manispaa hivyo atalifikisha katika vikao vya madiwani ili kuondoa kero hizo.

error: Content is protected !!