Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kubenea: CUF ndio wasaliti
Habari za Siasa

Kubenea: CUF ndio wasaliti

Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo
Spread the love

SIKU moja baada ya Chama cha Wananchi (CUF), kusisitiza kwamba hakitashirikiana na vyama vingine kutokana na kusalitiwa, Saed Kubenea amesema ‘CUF ndio wasaliti’. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kubenea ambaye ni mbunge wa Ubungo (Chadema), amemueleza mwandishi wa habari hizi, kwamba katika maisha yote ya siasa, CUF haikuwahi kuwa na mafanikio makubwa kama ilivyoshirikiana na muungano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Jana tarehe 23 Oktoba 2019, Jafari Mneke, Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi CUF, alituhumu vyama vya upinzani nchini kwamba vilikisaliti chama hicho.

“Tulisalitiwa…, Tunaingia kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa bila kushirikiana na chama chochote, kwasababu hatujaona chama chenye dhamira ya kweli ya kuiondoa CCM,” alisema Mneke.

Akizungumzia kauli hiyo Kubenea amesema, CUF iieleze ukweli umma kwamba iliingia kwenye mradi wa kuvuruga upinzani, “hawa waliingia kwenye mradi wa kuvuruga upinzani, hawataki kusema ukweli.”

Amesema, “madai kwamba CUF ilisalitiwa kwenye UKAWA au imesalitiwa, yanatolewa kwa ghiliba, hadaa, hila na kutaka kuficha ukweli.”

Mbunge huyo wa Ubungo ameeleza, kama CUF haitaeleza ukweli, UKAWA wataeleza ukweli huo kwa wananchi wakati wa kampeni kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2019.

“Kwanza tangu chama hicho kianzishwe, hakijawahi kupata mafanikio makubwa kama ilivyokuwa chini ya UKAWA, waache kusingizia watu, waseme ukweli kwamba huo ndio mradi waliokubaliana na CCM wa kuivuruga CUF na kuvunja umoja wa UKAWA.

“Waseme huo ukweli wananchi waelewe, wasiposema wao tutasema sisi, kwenye kampeni. Tutasema kwa wananchi CUF ni mdudu gani kwa wananchi,” amesema Kubenea.

Amesema, chaguzi zilizopita CUF ilipata wabunge 10 Bara, wanaongoza halmshauri, walipata Naibu Meya Manispaa ya Ilala, Ubungo na Kindononi,” amesema Kubenea na kuhoji “hapo wansemaje wamesalitiwa? Ni wakati gani walikuwa na mafanikio makubwa kuliko uchaguzi mkuu uliopita?”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!