Monday , 30 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kubenea: CCM inafanya mzaha msiichague
Habari za Siasa

Kubenea: CCM inafanya mzaha msiichague

Spread the love

SAED Kubenea, Mgombea Ubunge wa Kinondoni amesema, Serikali ya Chama Cha Mapimduzi (CCM), imefanya mzaha kwenye maisha ya watu kwa kuacha kujenga miondombinu ya maji Dar es Salaam na badala yake wanajenga Daraja la Coco Beach. Anaripoti Faki Sosi…(endelea)

Kubenea aliyasema hayo jana Jumapili tarehe 25 Oktoba 2020 kwenye kampeni ya Mtaa kwa Mtaa katika Kata ta Hananasif jimboni humo.

Kubenea alisema, Serikali inafanya mzaha na maisha ya watu badala ya kurekebisha miundombinu inayopelekea Dar es Salaam kuwa na mafuriko kila mvua inaponyesha yenyewe inajenga daraja.

Mwanasiasa huyo, aliyekuwa akitembea nyumba kwa nyumba kuomba kura akiwa mtaa wa soko la Hananasif aliwakutana na vijana, Wazee na Kina Mama aliwaomba kura wananchi hao huku akiwaeleza wamchague yeye akamalize matatizo ya Kinondoni pamoja na kumaliza kabisa changamoto ya mafuriko.

“Nichagueni, msiwachague CCM wanaacha kuboresha miundombinu ili kuyadhibiti mafuriko wanakwenda kujenga daraja la Coco ambalo linatumiwa na watu wachache huku wananchi masiki wakibaki kuhangaika mvua zinaponyesha,” alisema

Kubenea alikutana na makundi tofauti mtaani pamoja na watu wa CCM.

Katika kampeni za mtaa kwa mtaa Kubenea amekutana na Mwanachama wa Chama Cha Mapindu (CCM) aliyefahamika kwa jina moja la Juma aliyemueleza kura ya Ubunge atampa yeye lakini Kura ya Udiwani atampigia CCM.

“Mimi niwe mkweli tu, Ubunge nitakupa wewe (Kubenea) ila hao wa udiwani unaoniambia niwape siwezi kuwapa huyu aliyemaliza muda wake hakufanya jambo lolote la kimaendeleo,” alisema Juma akiibusha tabasamu kwa Kubenea na timu yake aliyokuwa akizunguka nayo

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chongolo asikitishwa na mradi wa Mil 900 kutoanza kutoa manufaa

Spread the loveKATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Spread the love  MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu:Suluhu ya ugumu wa maisha ni Katiba Mpya

Spread the love  MAKAMU mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Bara,...

error: Content is protected !!