April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kubenea azungumzia siku ya kuhama Chadema

Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo

Spread the love

SAED Kubenea, Mbunge wa Ubungo (Chadema) amesema, siku akitaka kuhama chama hicho, atasaema na si watu kupiga ramli. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Amesema, baadhi ya watu nje na ndani ya Chadema wamekuwa wakimchonganisha na viongozi wa chama hicho, na kwamba hajafikiria kuhama chama hicho kwa sasa.

“Sina mpango huo, sijapanga kuhama. Kama mpango wa kuhama utakuwepo, siku ikifika nitasema,” amesema na kuongeza “watu waache kunichonganisha.”

Kubenea ambaye ni rafiki wa karibu wa Anthony Komu, Mbunge wa Moshi Vijijini (Chadema), aliyetengaza kuhama chama hicho atapomaliza muhula wake, (Kubenea) anahusishwa kuungana naye kutokana na ukaribu wao.

“Urafiki wangu na Komu haimaanishi kila anachofanya nami nakifanya, kwa sababu ya urafiki wangu naye, lakini mpaka sasa hizo ramli ziachwe.

“Mimi bado mbunge wa Chadema Jimbo la Ubungo, ninadhani natakiwa kuendelea kutumikia wananchi wangu.  Waache tufanye kazi, muda ukifika tutazungumza hayo mambo kwa ujumla wake,” amesema Kubenea.

Akizungumzia kuhusu madai hayo, Kubenea amesema yanatokana na vita ya uchaguzi mkuu ujao, hususan kwa watu wanaoliwinda Jimbo la Ubungo.

“Inawezekana ni makundi yanayoibuka kwenye chama hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi. Hakuna mtu anayeweza kufikiri fulani simhitaji.

“Kwa mfano; nispogombea ubunge, mimi nina watu 10,000 katika jimbo nililofanya vizuri, hawawezi wakakupa kura wewe? ” amehoji Kubenea.

error: Content is protected !!