July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kubenea awatia kiwewe CCM

Spread the love

BAADHI ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wameonekana kuwa na wasiwasi kwa kitendo cha Mkurugenzi wa Mtendaji wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers, Saed Kubenea kupenya katika uchaguzi mkuu na kuingia bungeni. Anaandika Dany Tibason, Mpwapwa … (endelea).

Kwa masharti ya kutokutaka kutajwa majina makada hao walisema kuwa kutokana na umahiri wake wa kufanya kazi kubwa ya kiuchunguzi ni wazi kuwa ataweza kuiumbua serikali hasa katika mijadala mbalimbali.

“Akiwa katika kipindi chake cha uandishi alikuwa akiandika habari za uchambuzi na uchunguzi kwa kina na sasa kaingia bungeni hakika kutachimbika,” walisema makada hao.

Wakati huo huo baadhi ya wananchi wa Mpwapwa wameonesha furaha yao kwa ushindi wa Mbunge mteule wa jimbo la Mikumi, Joseph Haule (Chadema) maarufu kwa jina la Prof J.

Kwa nyanati tofauti wananchi hao wamesema kitendo cha nguli huyo wa mziki wa kizazi kipya kujitosa katika siasa ni ukombozi kwa vijana wenye vipaji mbalimbali.

Mmoja wa wananchi ambaye alizungumza na gazeti hili, Hawa Makau amesema mwimbaji huyo wa mziki wa kizazi kipya ni kati ya wanamuziki ambao wanajitambua.

Hawa amesema kutokana na hali hiyo ni wazi kuwa jimbo la Mikumi limepata mbunge ambaye kwa vyovyote vile ataweza kuinua vipaji vya wasanii wadogo na wakiunganisha nguvu yeye na Joseph Mbilinyi wataweza kupigania maslahi ya wasanii.

Naye Angela Mayoba amesema kitendo cha wanamuziki hao kuingia katika Bunge iwe chachu ya kukuza na kutetea maslahi ya wanamuziki wa nyimbo za injili pamoja na muziki mbalimbali.

Hata hivyo amesema umefika sasa wa jamii na wasanii wenyewe kujitambua na kuacha vitendo vya kutumia majukwaa kwa kujidhalilisha na badala yake watambue kuwa ni kazi kama ilivyo kazi nyingine ambayo inamjengea mtu heshima kama ilivyo kwa Joseph Haule na Sugu.

error: Content is protected !!