MBUNGE wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea, ameweka rehani mshahara wake wa mwezi huu, ikiwa Leo jioni wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wataweza kuzuia bajeti ya wizara ya Kilimo na Uvuvi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Akizungumza kwa hisia kali wakati akichangia bajeti ya wizara hiyo, Kubenea amesema, “hakuna mbunge hata mmoja ambaye anaweza kuzuia bajeti.”
Amesema, wabunge wa chama hicho ni dhaifu na hawana uwezo wa kusimamia mambo yao mpaka mwisho.
“Mheshimiwa Spika kama atasimama mbunge yeyote wa CCM na kutaka kukwamisha bajeti hii, natangaza mshahara wangu wa mwezi huu apewe akaongezee bajeti yake, huwa mnatupiga maneno tu bila vitendo,” amesema Kubenea.
Kubenea ametoa kauli hiyo leo bungeni katika mjadala wa bajeti hiyo, kubainisha kuwa wabunge wa CCM wamekuwa wakipitisha kwa nguvu bajeti baada ya kuitwa kwenye vikao vya ndani vya chama hicho.
Baada ya Kubenea kueleza hayo, baadaye Spika wa Bunge, Job Ndugai aliwatangazia wabunge wa chama hicho tawala kuwa watakuwa na kikao cha ndani kitakachofanyika katika ukumbi wa White House, kabla ya kurejea tena bungeni saa 10 jioni.
Mara nyingi hoja za wabunge zinapokuwa moto bungeni kuhusu wizara fulani, CCM huitisha vikao hivyo vya ndani.
Amesema ni aibu kwa Serikali kuendelea kuagiza nyama, kuku na samaki kutoka nje ya nchi wakati vitu hivyo vimejaa nchini.
Leave a comment