Friday , 1 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kubenea aukataa mpango wa uchumi
Habari za SiasaTangulizi

Kubenea aukataa mpango wa uchumi

Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo
Spread the love

MBUNGE wa Ubungo Saed Kubenea (Chadema) ameiponda taarifa ya hali ya uchumi 2016 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2017/18, anaandika Dany Tibason.

Kubenea amesema kuwa licha ya bajeti kuonekana kuwa imeongezeka lakini haina maana kuwa hiyo ni bajeti yenye uhalisia na badala yake kinachoonekana kuongezeka ni kuongeza takwimu.

Akizungumza na MwanaHALISI Online katika mahojiano maalumu juu ya kuongezeka kwa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18 amesema kuwa serikali imeongeza takwimu ili kuonesha kuwa bajeti ni kubwa lakini hakuna uhalisia wowote.

Mbunge huyo amesema kwamba serikali haijawai kupeleka pesa za maendeleo kwa wakati jambo ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa kushindwa kufikia malengo ya kimaendeleo.

Mbali na hilo Kubenea ameeleza kwamba kwa sasa katika serikali ya awamu ya tano kuna mambo mengi yanafanyika lakini hayatoi mwanya wa kuwashirikisha wabunge au wananchi kwa ujumla wake.

Akizungumzia masuala ya ununuzi wa ndege, pamoja na ujenzi wa reli amesema sheria za manunuzi hazijafuatwa kwani hakuna hata sehemu moja ambapo lilitolea tangazo la tenda ya ununuzi wa ndege au ujenzi wa reli.

“Yapo mambo ambayo yanatolewa maamuzi na mtu mmoja jambo ambalo linakiuka sheria ya manunuzi, kuna mambo ambayo lazima yazingatie utawala bora na uwazi na ushirikishwaji kwa wananchi kwa ujumla.

“Tunaweza kujiuliza katika suala la ununuzi wa ndege nani walioshirikishwa, lakini pia katika ujenzi wa reli nani walioshirikishwa wapi zabuni zimetangazwa na nani walioshindanishwa lakini tunashuhudia watu wakiendelea kufanya kazi kujenga reli makampuni kutoka nje na mambo mengine kama hayo kutoka na hali hiyo bajeti ya serikali haiwezi kuwa na uhalisia ya kibajeti,” ameeleza Kubenea.

Naye mbunge wa Nzega Mjini, Husein Bashe (CCM) amesema ili kufanikisha bajeti iwe nzuri na manufaa kwa jamii ni kuondoa kodi ambayo ni kero kwa jamii.

Mbali na kuondoa kodi pia amesema ni jambo jema kuboresha sekta ya kilimo, kutoa kipaumbele kwa miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kukuza uchumi kwa mtu moja moja badala ya kuhesabu uchumi kukua kwa njia ya ghafla tu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mwili wa Hayati Mwinyi kuagwa leo saa 8 Uwanja wa Uhuru

Spread the loveMWILI wa Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi unatarajiwa kuagwa kuanza...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi kuzikwa Machi 2 visiwani Unguja

Spread the loveMWILI wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania,...

Habari za SiasaTangulizi

Rais mstaafu Mwinyi afariki dunia

Spread the loveRais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan...

Habari za Siasa

Waziri mkuu Ethiopia atua Tanzania

Spread the loveWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia,...

error: Content is protected !!