July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kubenea atoa ahadi nzito Ubungo

Spread the love

MBUNGE wa Ubungo na Mkurugenzi wa Hali Halisi Publishers, Saed Kubenea (Chadema) amewahakikishia wakazi wa jimbo la Ubungo kuwa atawapatia maendeleo katika jimbo hilo. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Mbali na hilo amewapongeza waandishi wa habari kwa kushirikiana naye katika kufichua maovu ambayo yalipangwa kufanywa na serikali ya CCM kuwapora wapinzani ushindi.

Kubenea alitoa kauli hiyo jana mjini hapa baada ya kuapishwa kuwa mbunge wa jimbo hilo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Ubungo zaidi ya 500 waliomsindikiza kwa ajili ya kushuhudia jinsi anavyoapishwa.

Kubenea akizungumza na umati wa wananchi hao amesema katika jimbo hilo atapambana na wafanyakazi wazembe na legelege.

“Natangaza kuwa wakurugenzi ambao wanasababisha uzembe na kudorora kwa maendeleo hakika tutapambana nao ili kuondoa dhana ya kulindana.

“Tutaunda halmasahauri yenye nguvu ambayo lengo kubwa ni kuhakikisha maendeleo yanawafikia wananchi wote bila juwepo kwa ubaguzi,” amesema Kubenea.

Akizungumzia suala la madereva bodaboda, amesema baada ya kuunda halmashauri madereva wa bodaboda watatungiwa sheria ya kufika katikati ya mji tofauti na ilivyo sasa.

“Hatuwezi kukubali kuona vijana wetu wakihangaika wakati wanatakiwa kuwezeshwa kufanya kazi zao kwa ajili ya kujipatia kipato,” amesema Kubenea.

Pamoja na mambo mengine Kubenea amesema yeye amefika bungeni kutokana na nguvu ya umma, hivyo hatapandisha mabega kwa kuwabeza wananchi.

Akizungumzia kuhusu kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo (Chadema), Kubenea amesema ni jambo la kulaaniwa kwa kifo chake ambacho kinahusishwa na wafuasi wa CCM.

error: Content is protected !!