July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kubenea ataka waliotoa vibali maeneo ya wazi wawajibishwe

Spread the love

MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema), ameitaka serikali kutowaacha wahusika waliotoa vibali vya ujenzi katika maeneo ya wazi na yale yasiyoruhusiwa ambayo sasa waliojenga wanaathirika na bomoabomoa. Anaandika Josephat Isango … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Manispaa ya Kinondoni, Kubenea amesema kitendo cha kubomoa nyumba za wananchi ambao wengine wana vibali vya serikali ni kuwaonea wakati wahusika waliowafikisha hapa wamo.

Katika bomoaboma hiyo iliyoanza Novemba 18 hadi 20 na kusimamiwa na Halmashauri ya Kinondoni, ilibomoa jumla ya nyumba 20.

Amesema bila ya kufanya hivyo serikali ya CCM itaendelea kujenga utamaduni kwa watumishi wa umma kuruhusu ujenzi holela kwa ajili ya kunufaisa matumbo yao halafu mwisho wa siku wanaoumia ni wananchi ambao wamejinyima na kujenga nyumba.

Aliongeza kuwa endapo serikali haitakuwa makini katika kushughulikia suala hili itajikuta baadaye ikilipa fidia, fedha ambazo ni kodi za wananchi.

Fedha hizo Kubenea amesema zingeweza kuwekeza katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo elimu na afya, maeneo ambayo yamekuwa na changamoto kubwa katika utendaji wa serikali.

Kwa mujibu wa Mbunge huyo amesema amelazimika kulisemea hilo baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wakazi mbalimbali walioathirika na zoezi hilo ambao anatarajia kukutana nao leo na kuona vielelezo vyao.

“Jamani hili sula la bomoabomoa liangalie pande zote kwa watumishi wa serikali pia ni mahala panapotakiwa kumulikwa kwa kuwa haingii akilini kwamba mwananchi mwenyewe anaweza kuingia mahala na kunza kujenga nyumba ya gharama kubwa bila ya kuthibitishwa na mamlaka husika,” amesema.

error: Content is protected !!