Saturday , 15 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kubenea ataka Tume Huru kabla ya 2020, amuomba Prof. Kabudi amuunge mkono
Habari za SiasaTangulizi

Kubenea ataka Tume Huru kabla ya 2020, amuomba Prof. Kabudi amuunge mkono

Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Picha ndogo, Waziri wa Sheria na Katiba Prof. Paramagamba Kabudi
Spread the love

SAED Kubenea, Mbunge wa Ubungo, amewasilisha hoja binafsi Bungeni ili kupata Tume Huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2020, huku akimtwisha zigo Waziri wa Sheria na Katiba Prof. Paramagamba Kabudi kubeba hoja yake. Anaandika Mwandishi Wetu … (endelea).

Kubenea amewaambia waandishi wa habari leo kuwa, aliwasilisha barua yake Machi 8, mwaka huu, kwa Katibu wa Bunge kwa kutumia Kanuni ya 55 (1) na (2), pamoja na Kanuni ya 54 (1) (2) na (3) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, toleo la Januari 2016 inayompa mamlaka mbunge kuwasilisha hoja binafsi bungeni.

Mbunge huyo wa Ubungo amesema lengo lake la kupeleka hoja binafsi ni kutokana na kutokuwepo kwa tume huru itakayoweza kujiendesha yenyewe mambo yake bila ya kutegemea kupata msaada serikali huku akitolea mfano suala la bajeti la kuendesha tume wakati wa chaguzi.

Kubenea amesema Tume ya Uchaguzi ya sasa haiwezi kuwa huru kutokana na sababu mbalimbali zilizokuwemo katika muundo wa tume hiyo, hivyo nimewasilisha hoja yangu ili Bunge ijadili na kuitaka serikali kuleta muswada wa kurekebisha katiba kwa lengo la kupatikana kwa tume huru.

“Baada ya kuwasilisha hoja yangu, Bunge lijadili na kuazimia serikali ipeleke Bungeni mswada wa marekebisho ya Katiba ili kuruhusu kuundwa kwa chombo huru kitakachoweza kusimamia uchaguzi kitachoitwa Tume Huru ya Uchaguzi,” amesema Kubenea.

Kubenea amesema Tume ya Uchaguzi ya sasa ni kilio cha watu wengi, wakiwemo viongozi wakuu wa Serikali, Vyama vya Siasa, Asasi za Kiraia wote kwa nyakati tofauti wamekuwa wakitaka Tume Huru ya Uchaguzi, hivyo ana imani ataungwa mkono na wadau mbalimbali kufanikiwa hilo.

“Kilio cha kupata Tume Huru ya Uchaguzi hakijaanza leo, ni cha miaka nenda rudi. Hivyo naamini nitaungwa mkono na wadau wengi ili Taifa hili liweze kupata tume huru kabla ya uchaguzi mkuu wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji wa mwaka 2019 na Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2020,” amesema Kubenea.

Kubenea amesema madai ya kupatikana kwa tume huru ya uchaguzi yalianza hata kabla ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya Siasa mwaka 1992, lakini hadi sasa haijapatikana.

“Malalamiko ya Tume Huru ya Uchaguzi siyo yangu peke yangu na hayajaanza leo. Tume ya Jaji Francis Nyalali iliyoundwa 1991, ilipendekeza Mfumo wa Vyama Vingi na Tume Huru ya Uchaguzi. Mfuno umekubaliwa lakini Tume Huru imegomewa,” amesema Kubenea na kuongeza:

“Tume ya Jaji Robert Kisanga iliyoundwa mwaka 1999 ilisema hatua ya wajumbe wa Tume kuteuliwa na Rais ambaye aweza kuwa kiongozi wa chama kinachotawala, katika utendaji wao ama watakuwa na upendeleo kwa chama husika au watalipa fadhila kwa aliyewateuwa.

“Ripoti ya Tume Mabadililo ya Katiba ya Jaji Joseph Warioba huku Prof. Paramaganda Kabudi ambaye sasa ni Waziri wa Sheria na Katiba akiwa kamishna wake, na hata Rasimu yenyewe ya Katiba iliyoandaliwa na Tume hiyo, imeeleza kwa mapana umuhimu wa kubadili muundo wa Tume ya Uchaguzi na kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi.”

Kubenea amesema hoja yangu nina imani Prof. Kabudi anaijua vizuri sana kwani aliishia wakati akiwa kamishna wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, hivyo sasa akiwa Waziri wa Sheria na Katiba wa serikali ya Rais John Magufuli ni wakati wa kuishawishi serikali kuja na maadhimio ya mabadiliko ya Katiba ili kuipata Tume Huru ya Uchaguzi.

Kubenea amesema kwa mfumo wa sasa wa Tume ya Uchaguzi, unapokuwa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Mkurugenzi na Makamishna wengine wameteuliwa na Rais ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha siasa aliyekuwa katika ushindani wa vyama vingine, inawezaje kutenda haki.

“Kuwa na Tume ya Uchaguzi ambayo inaundwa na viongozi walioteuliwa na Rais ambaye ni mshindani katika uchaguzi mnaoshiriki, hapo hakuna uchaguzi bali kuna uchakachuwaji wa uchaguzi,” amesema Kubenea.

Kubenea akaongeza kuwa kitendo cha wakurugenzi wa Halmashauri za Miji, Manispaa, na wilaya ndiyo wasimamizi wa Uchaguzi, kwani hawa mbali ya kuwa wateule wa Rais, wengi wao ni makada wa CCM, hivyo tunataka sheria mpya itakayoondoa makada wa Vyama vya Siasa kusimamia uchaguzi.

Mbunge huyo amesema matarajio yake Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai atatumia busara zake zote na mamlaka aliyopewa ili kuruhusu hoja aliyoipeleka Bungeni ipite na izae matunda mazuri ndani yake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Rais Samia amng’oa Matinyi Serikalini, ateua viongozi mbalimbali

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali akiwamo...

BiasharaHabari za Siasa

Tanesco yawasha mtambo namba 8 Bwawa Julius Nyerere

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Samia: Wakuu wa mikoa, wilaya wanaendeleza ubabe

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema bado wakuu wa wilaya na...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Ramaphosa achaguliwa tena kuwa rais Afrika Kusini

Spread the loveRais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amechaguliwa na wabunge wa...

error: Content is protected !!