December 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kubenea ashinda rufaa, kurejea kwa kushindo

Spread the love

KAMATI ya Maadili ya Kitaifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania, imetengua uamuzi wa kamati ya maadili Jimbo la Kinondoni iliyomfungia siku saba kufanya kampeni, mgombea ubunge wa Jimbo hilo kupitia ACT-Wazalendo, Saed Kubenea. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Tarehe 20 Oktoba 2020, Kamati ya Maadili Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam, ilimfungia Kubenea kwa siku saba kuanzia 21 hadi 27 Oktoba 2020 akituhumiwa kutoa lugha zisizotakiwa dhidi ya mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Baada ya adhabu hiyo, Kubenea aliyewahi kuwa mbunge wa Ubungo jijini humo kupitia Chadema kati ya mwaka 2015 hadi 2020, alikata rufaa Kamati ya Maadili ya Kitaifa akipinga kufungiwa.

Leo Jumamosi tarehe 24 Oktoba ikiwa ni siku tatu zimepita tangu kufungiwa, kamati hiyo imemrejesha ulingoni kuendelea na kampeni za Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano ijayo 28 Oktoba 2020.

Akizungumzia uamuzi huo wa kurejeshwa kwake, Kubenea ameishukuru kamati hiyo kwa kumtendea haki kwa kumrejesha huku akisema “nianaza kampeni leoleo, Magomeni na kehso nitafanya kampeni katika kata nne kuhiutimisha kata 10 za Jimbo la Kinondoni na Jumanne nitafunga kampeni kwa kishindo.”

error: Content is protected !!