Saturday , 10 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kubenea apigania kurejeshwa Kiwanda cha Urafiki
Habari za Siasa

Kubenea apigania kurejeshwa Kiwanda cha Urafiki

Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo
Spread the love

SAED Kubenea, Mbunge wa Ubungo (Chadema) ameihoji serikali kwamba, ni lini itafufua nakuwa imara zaidi Kiwanda cha Urafiki ili kifanye kazi kwa maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla kama ilivyokusudiwa? Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Akizungumza bungeni leo tarehe 8 Februari 2019 Kubenea amesema, kiwanda hicho cha nguo kilichopo katika Jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam ni miongoni mwa viwanda vilivyobinafsishwa na serikali.

“Katika kiwanda cha nguo cha Urafiki mwekezaji hakuja na mtaji badala yake serikali ilienda kukopa katika Benki ya Exim ya China na ikampa mwekezaji mtaji wa kuendesha Kiwanda cha Urafiki mikononi mwa wananchi wa Dar es Salaam,” amesema.

Akijibu swali hilo Injinia Stella Manyanya, Waziri wa Viwanda na Biashara amesema, kiwanda hicho msingi wake ni uhusiano kati ta China na Tanzania.

“Kama ambavyo amezungumza Kiwanda cha Urafiki ni uhusiano kati ya Nchi ya China na Tanzania. Ni kiwanda ambacho kilijengwa msingi wake ni mahusiano ya nchi hizo mbili kidiplomasia.

“Hivyo basi, tunatamani kuona kiwanda hicho kikifanya kazi vizuri zaidi na wote tumefuatilia na kujua maeneo yanayohitajika kufanyiwa marekebisho,” amesema Injinia Manyanya.

Amesema, kuwa serikali zote mbili zinashughulika kwa pamoja kuona namna gani kiwanda hicho kinaweza kuendeshwa kisasa zaidi.

Waziri huyo amesema, katika kujenga uchumi wa viwanda, Serikali ya Awamu ya Tano tangu iingie madarakani hadi kufikia Desemba Mwaka 2018, jumla ya viwanda 3,504 vimeanzishwa nchini.

Amefafanua kuwa, viwanda hivyo vinajumuisha viwanda vidogo sana 2500, viwanda vidogo 943, viwanda vya kati 51 na viwanda vikubwa 10.

“Wizara yangu kwa kushirikiana na Ofisi ya Msjili wa Hazina imekuwa ikifanya tathmini ya viwanda 156 vilivyobinafsishwa na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa kwa viwanda 68 ambavyo havijaendelezwa.

“Hatua hiyo ni kuwa, tayari viwanda 14 vimerejeshwa serikalini na juhudi za kuvitafutia wawekezaji wengine walio tayari kuviendeleza zinaendelea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lussu: Mkataba wa DP bandarini si wa miaka 100

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema hakuna ukweli wowote...

Habari za SiasaTangulizi

Maulid Mtulia: Kutoka ubunge hadi U-DAS

Spread the love ALIYEKUWA mbunge wa Kinondoni, kupitia vyama vya The Civil...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

error: Content is protected !!