July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kubenea aongoza promosheni ya MwanaHALISI

Spread the love

MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Hali HALISI Publishers, Saed Kubenea leo ameungana na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa kufanya promosheni ya kutangaza gazeti la MwanaHalisi barabarani ikiwa ni toleo la kwanza baada ya kutoka kifungoni. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Promosheni hiyo imefanyika katika maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na Barabara ya Morogoro sehemu za Magomeni na Ubungo pia katika makutano ya Barabara ya Sam Mujoma na Old Bagamoyo (Mwenge).

Miongoni mwa waliojumuika kwenye promosheni hiyo ni pamoja na Meneja Mkuu wa Hali Halisi, Robert Katula; Mkurugenzi wa Utawala na Fedha, Yusuf Aboud pamoja na idara zingine kwenye kampuni hiyo.

Kazi hiyo ilianza saa 2:30 asubuhi ambapo wafanyakazi hao waliongozana kwa pamoja na kuuza magazeti kwa pamoja na kuhama kituo kila baada ya dakika 30.

Hali ilivyokuwa barabarani.

Wakati timu hiyo ya wafanyakazi wakiongozana na Kubenea huku wakiwa wameshika magezeti hayo, wananchi waliyapokea kwa shauku wakiwa na furaha kutokana na kuanza kuchapishwa kwa gazeti hilo.

“Bora gazeti letu hili limerudi maana ‘tulizi-miss’ stori za uchunguzi na za uhakika, tena wamelifungulia muda muafaka. Tunaishukuru mahakama kwa uamuzi sahihi, lakini na kipato kwangu kitazidi,” alisema John Simion ambaye ni muuza magazeti Kituo cha Daladala Magomeni Usalama.

Gazeti la MwanaHALISI limekuwa kifungoni kwa muda wa miaka mitatu, mwezi mmoja na siku 35. Lilifungwa kwa kufutiaa tangazo la serikali Na. 258 la tarehe 27 Julai, 2012.

Hata hivyo, Septemba 4 mwaka huu Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilitoa hukumu na kuliacha huru gazeti hilo kwa maelezo kuwa “serikali ilikosea kufuata taratibu.”

Wakati wa kufunga gazeti hilo, Waziri wa Habari, Michezo na Utamaduni, Dk. Fenella Mukangara alitangaza kufunga gazeti hilo kwa muda usiojulikana kwa maelezo kuwa linachapisha makala za uchochezi.

error: Content is protected !!