Monday , 27 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kubenea amtoa jasho Mwijage bungeni
Habari za Siasa

Kubenea amtoa jasho Mwijage bungeni

Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo. Picha ndogo Charles Mwijage Waziri wa Viwanda
Spread the love

WAZIRI wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage alijikuta katika wakati mgumu baada ya kushindwa kujibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema), anaandika Dany Tibason.

Mwijage alijikuta akipiga siasa na kutoa majibu yaliyoelezwa kuwa ni ya uchochezi kwa wapiga kura wa jimbo la Ubungo badala ya kushindwa kutoa majibu sahihi kama alivyouliza muuliza swali la nyongeza ambaye ni Kubenea.

Katika swali la nyongeza Kubenea alitaka serikali ieleze ni lini itaweza kutatua migogoro ambayo inajitokeza katika viwanda ambavyo vipo Ubungo kutokana na wafanyakazi kutolipwa mishahara yao kwa wakati.

Kubenea mesema uwekezaji hauendani na matakwa yanayotakiwa na kuuliza ni lini serikali itaweza kutatia migogoro mikubwa kati ya wawekezaji wa kiwanda cha Urafiki kutokana na kuwepo kwa malalamiko kwa wafanyakazi kutolipwa mishahara kwa wakati.

Awali katika swali la msingi la mbunge wa Viti Maalum, Mwanne Mchemba (CCM) alitaka kujua ni lini serikali italeta wawekezaji katika mkoa wa Tabora.

“Mkoa wa Tabora upo tayari kwa ajili ya uwekezaji wa EPZ uliotengewa eneo katika wilaya ya Uyui, Je ni lini serikali italeta wawekezaji katika mkoa wa Tabora?” alihoji.

Akijibu swali la nyongeza la Kubenea, Charles Mwijage, amesema viwanda vilivyopo Ubungo vinaweza kuajili vijana zaidi ya 400.

“Kama viwanda vilivyopo ubungo nilitamani kuviamishia katika jimbo langu kwani viwanda hivyo ni mtaji mkubwa kwa wapiga kura wa Ubungo hivyo viwanda hivyo vinaweza kuajiri vijana zaidi ya 400”  amesema Mwijage.

Amesema mchakato wa kutenga eneo mkoa wa Tabora kwa ajili ya EPZ ulianza mwaka 2010 baada ya wizara kuelekeza uongozi wa mkoa kutenga eneo lisilopungua ukubwa wa hekari 2,000.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kasekenya aipa Tanroads wiki kukarabati barabara Morogoro

Spread the loveNaibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ametoa wiki moja...

Habari za SiasaTangulizi

‘Aliyemtonya’ Lissu kuhusu rushwa arejea madarakani

Spread the loveMwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Iringa, William Mungai...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Tutaendelea kupigania malengo ya afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema dhamira ya Tanzania...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NHC yadai bil. 2.1 taasisi za Serikali, Waziri atoa maagizo

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii...

error: Content is protected !!