July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kubenea amkana Makonda kortini

Spread the love

SAED Kubenea, Mbunge wa Jimbo la Ubungo pia Mkurugenzi wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers amekana kumtusi Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, anaandika Faki Sosi.

Kubenea amekana kumtukana Makonda leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Slaam wakati akitoa ushahidi wa kesi inayomkabili kufanya hivyo iliyofunguliwa tarehe 15 Desemba mwaka jana.

Kwenye kesi hiyo, Kubenea alifunguliwa madai matatu ambayo ni lugha ya matusi, kumwita Makonda mpumbavu, mjinga pamoja na cheo cha kupewa.

Katika kesi hiyo iliyopo mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba ambayo Kubenea alionekana kuwa na kesi ya kujibu, imeanza kusikilizwa leo baada ya mbunge huyo kuanza kutoa ushahidi wake.

Kubenea ndiye shahidi namba moja kwenye kesi hiyo ambapo ameieleza mahakama kwamba, katika vuta nikuvute iliyotokea tarehe 14 Desemba mwaka jana kwenye Kiwanda cha nguo cha TOOKU kilichopo Ubungo, jijini Dar es Salaam hakumtukana Makonda na kwamba, hatua ya kumkatalia kuzungumza na wananchi hakikuwa kitendo cha kiungwana.

Peter Kibatala wakili mtetezi wa Kubenea alimtaka (Kubenea) asimulie kilichotokea kwenye mkutano huo.

Kubenea aliieleza mahakama kuwa alifika kwenye kiwanda hicho ili kutafuta suluhu ya mgogoro ulikuwepo kwenye kiwanda hicho.

Na kwamba, uongozi wa kiwanda hicho ulikubali kuongeza mshahara kwa wafanyakazi hao kwa asilimia tano kutoka kwenye Sh. 100,000 hadi 100,5000.

Kubenea aliieleza mahakama kwamba, wakiwa kwenye mkutano huo ving’ora lisikika baadaye walitoka wote walikuwa kwenye mkutano huo na kuwaona askari polisi wakiwa kwenye gari yao na gari nyingine akiwemo Makonda.

Alieleza kuwa, Makonda aliingia kwenye mkutano huo wakati muafaka haujapatikana. Kisha Makonda aliwaamuru watoke nje walipo wafanyakazi.

Wakati huo walikuwa wakivutana ambao Kubenea alisema, walikubaliana kwenda walipo wafanyakazi nje ya chumba ambacho mkutano ulikuwa ukifanyika.

Kubenea alieleza kuwa, alianza kupewa nafasi Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa unaozunguka kiwanda hicho na baadaye wafanyakazi.

Baada ya wafanyakazi, alisimama Makonda na kusema kuwa yeye amewasikiliza na kwamba, atawaita Waziri wa Ajira, Kazi na Vijana pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara katika siku iliyofuata.

Kubenea aliiambia mahakama kwamba, Makonda alifunga mkutano na kuwaaga ambapo yeye (Kubenea) alimuomba asifunge mkutano huo ili naye aongee na wafanyakazi.

Anasimulia kwamba, Makonda alimjibu kuwa yeye ndiye msemaji wa mwisho na sehemu yoyote anapokuwepo yeye hawezi mtu mwengine kuongea na kwamba yeye ndiye Rais wa Kinondoni.

Kubenea ameieleza mahakama kuwa, yeye na Makonda hawana maeleweno mazuri baada ya kuulizwa swali na Kishenyi Mutalemwa, Wakili wa Serikali.

Kwamba, Kubenea aliandika habari iliyohusu kuhusika kwa Makonda kumpiga Jaji Mstaafu Joseph Warioba, aliyekuwa Mweyekiti wa Tume ya Katiba Mpya kwa kuwatumia vijana.

Mtalemwa: Je, Makonda aliwahi kufungua kesi ya kashfa dhidi yako.

Kubenea: Hapana.

Mutalemwa: Je, utakubaliana na mimi kuwa Mheshimiwa Makonda hakufungua kesi kwa sababu alijua utashindwa?

Kubenea: Hapana alishindwa kufungua kesi kwa sabubu aliogopa kutokana na kuwa, nilikuwa na ushahidi wa yeye ndio muhusika kwenye kumpiga Warioba.

Mutalemwa: Je, wafanyakazi au kiwanda wapo kwenye jimbo gain?

Kubenea: Kwenye Jimbo la Ubungo

Mutalemwa: Ulisema kuwa mlitofautiana na Makonda baada ya kusema kuwa mtoke mkaonge na wafanya kazi.

Kubenea: Ndio.

Mutalemwa: Kwanini mlitofautiana?

Kubenea: Kwa sababu tulikuwa hatujapata muafaka ambao tungeweza kuupata kwa mazungumzo kwenye mkutano wa ndani na kwamba, mazungumzo yalikuwa hayajaisha.

Mutalemwa: Uliumia sana baada ya kunyimwa nafasi ya kuongea na wafanyakazi.

Kubenea: Ndio.

Mutalemwa: Kwanini uliumia?

Kubenea: Kwa sababu mimi nilikuwa pale tangu asubuhi ili kuhakikisha kuwa mgogoro unaisha nikiwa kama mbunge wao.

Mutalemwa: Unahisi Makonda alimaanisha nini kusema kuwa yeye hakwenda kuomba kura.

Kubenea: Alikuwa amenipiga kijembe mimi na alimaanisha kuwa mimi nilikwenda kufanya siasa.

Peter Kibatala, wakili wa mshitakiwa aliiomba mahakama kuwa kuna shahidi muhimu ambaye akikosa kutoa ushahidi wakati huo hatopatikana ambapo mahakama ilikubali ombi hilo na kuruhusiwa kutoa ushahidi shahidi huyo.

Shahidi huyo ni Boniphace Nyenyembe, Katibu Msaidizi wa Chama cha Wafanyakazi Kinondoni aliieleza mahakama kuwa, yeye alishudia na kwamba haukuumsikia Kubenea akitoa lugha ya matusi.

Aliieeleza mahakama kuwa, yeye alifuatwa na wakili na Makonda na kumuuomba akatoe ushahidi upande wake ambapo alishindwa kumtumia kwenye kesi hiyo.

Nyenyembe amesema kuwa, alimsikia Makonda akijinadi kuwa yeye ndio Rais wa Kinondoni na kwamba, hakuna mtu yoyote anayeweza kuongea baada yake.

Amesema, Kubenea alisikia akilalamikia kuwa, yupo hapo tangu asubuhi kwanini hakumoa nafasi ya kuongea.

Ameieleza mahakama kuwa, alimsikia Kubenea akisema yeye sio ‘kibaka’ wala sio mvamizi kwenye mkutano huo.

error: Content is protected !!