Sunday , 2 April 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kubenea akagua ukarabati wa shule
Habari za Siasa

Kubenea akagua ukarabati wa shule

Spread the love

SAED Kubenea, Mbunge wa Ubungo (Chadema), amefanya ziara ya ukaguzi wa ukarabati wa Shule za Msingi Mabibo na Makuburi zilizopo jimboni mwake, anaandika Faki Sosi.

Shule hizo zinakarabatiwa kwa fedha kutoka Halmashauri ya Ubungo na mfuko wa mbunge huyo ambazo zote zinakaribia kufikia Sh. 90 milioni.

Mfuko wa mbunge umetoa Sh. 17 milioni kwa ajili ya kukarabati shule ya msingi Makuburi.

Ukarabati huo ni wa majengo matano ya Shule ya Mabibo inayowekwa mabati mapya kutoka vigae ambavyo vimeharibika gharama yake ni Sh. milioni 17 kutoka mfuko wa jimbo wa Mbunge na ukarabati wa madarasa Shule ya Makuburi Sh. 40 milioni na Sh. 32 milioni zinazotumika kujenga vyoo.

Katika ziara hiyo, Kubenea aliambatana na Ofisa Mtendaji Kata ya Makuburi na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa ya Mwongozo zilipo shule hizo mbili pamoja na wajumbe wa Kamati za Shule.

Kubenea ametembelea darasa la tatu la Shule ya Makuburi na kuwaahidi wanafunzi watano watakaofanya vizuri katika mtihani wao wa taifa wa darasa la nne mwakani atawazawadi Sh. 100,000 kila mmoja.

Wakati huo huo Kubenea amewasalimu walimu wa shule hizo pamoja na wanafunzi hao ambao amewasisitiza kusoma kwa bidii ili siku moja waje wawe wabunge, walimu, wanasheria na wahandisi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia apangua mawaziri

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la...

Habari za Siasa

RC mstaafu afariki dunia, CCM yamlilia

Spread the loveALIYEWAHI kuwa mkuu wa mikoa ya Dodoma, Mara, Mtwara na...

Habari za Siasa

Marekani kuwekeza Dola 500 Mil kupeleka bidhaa na huduma Tanzania

Spread the loveMAKAMU wa Rais wa Marekani, Kamala Harris amesema miongoni mwa...

Habari za Siasa

Kamala ataja hatua mpya kuimarisha uhusiano wa kibiashara Tanzania, Marekani

Spread the loveKATIKA kuimaridha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi baina ya Tanzania...

error: Content is protected !!