August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kubenea atetea Morogoro

Spread the love

WAKATI Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa ikipitisha Sh. 296 bilioni za makadirio ya bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 kwa Mkoa wa Morogoro leo, Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo amesema fedha hizo ni kidogo, anaandika Pendo Omary.

Akiwasilisha makadirio hayo, Dk. Steven Kebwe, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro amesema mkoa wake unatarajia kutumia jumla ya shilingi 296 bilioni, huku fedha za matumizi ya kawaida zikiwa 240 bilioni, matumizi ya maendeleo ya ndani zikiwa Sh. 32 bilioni na miradi ya nje zikiwa ni Sh. 23 bilioni.

Kubenea amesema, bado fedha zilizotegwa kwa maendeleo ni kidogo ukilinganisha na fedha za matumizi ya kawaida.

“Fedha za maendeleo kwa bajeti nzima ni asilimia 19 huku matumizi ya kawaida zikiwa 81 wakati serikali imesema mwaka huu fedha za maendeleo zitakuwa ni asilimia 40 ya bajeti. Napendekeza fedha za maendeleo walau zifike asilimia 20,” amesema Kubenea.

Magreth Sitta, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo amesema viongozi wa mkoa huo wanapaswa kuanisha mkakati madhubuti wa kibajeti katika kuhakikisha wanamaliza migogoro ya ardhi kati ya wafugaji na wakulima.

“Upimaji wa matumizi bora ya ardhi ulipaswa kuwa kipaumbele katika bajeti. Ni lazima mhakikishe mnakuja na mikakati ya kukomesha kabisa tatizo,” amesema Sitta.

error: Content is protected !!