July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kubenea aishiwa uvumilivu

Spread the love

SAED Kubenea, Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema) amepanga kutoa taarifa itakayowagusa viongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais John Magufuli na Jeshi la Polisi, anaandika Faki Sosi.

Kwenye taarifa hiyo pia ataeleza taarifa za kukamatwa kwake zilizothibitishwa na Simon Siro, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Taarifa kwenye vyombo vya habari jana zilieleza kwamba, Kubenea ni miongoni mwa waliokamatwa na Jeshi la Polisi ambapo Kamanda Siro alidai kukamatwa kwake.

Taarifa kutoka ndani ya Chadema zinaeleza kuwa, anatarajia kutoa taarifa kwa umma wakati wowote kueleza kile kinachoitwa sakata la polisi, madiwani na wabunge wa Ukawa wakati wa vurugu za uchaguzi wa meya ulioghairisha Jumamosi wiki iliyopita.

Taarifa kutoka kwa mmoja wa viongozi wa juu wa Ukawa inaeleza kuwa, Kubenea anatarajia kutoa taarifa ili kutoa ufafanuzi wa ndani kuhusu tukio hilo.

“Kubenea atatoa taarifa muda wowote kuanzia sasa, kwa kuongea moja kwa moja na waandishi wa habari, ama kutoa taarifa kwa vyombo vya habari,” amesema.

error: Content is protected !!