July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kubenea aibuka kidedea kura za maoni Ubungo

Mgombea wa Ubunge Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya Chadema, Saed Kubenea (katikati) akishuhudia bonanza la mpira wa miguu Kibamba muda mfupi baada ya kushinda kura ya maoni

Spread the love

MTIA nia wa Ubunge Jimbo la ubungo kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Saed Kubenea ameibuka kidedea katika kura za maoni baada ya kuwagaragaza vibaya wapinzani wake. Anaandika Jimmy Mfuru … (endelea).

Katika motokeo hayo kwa kishindo Kubenea amewaacha mbali wenzake kwa kupata kura 61 huku anaefuatia Goodluck Mollel akiambulia kura 20 na Gudat Lehad aliyeshika mkia amepata kura nne.

Kura za Kibamba na Ubungo zimefanyika katika ukumbini wa Happy Forest Kimara Baruti Jijini Dar es Salaam ambamo Kubenea amejipatia ushindi huo kwa kishindo.

Hivi karibuni Kubenea aliamua kuvunja ukimya baada ya uvumi kuenea kuwa alikuwa na nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Mafia mkoa wa Pwani baada ya kuchukua fomu rasmi kugombea ubunge Jimbo Ubungo.

Kubenea ambaye ni Mwandishi Mkongwe wa Habari za Uchunguzi amejizolea umaarufu baada ya kutunukiwa tuzo ya Shujaa kati yetu katika kipengele cha Uwazi na Ukweli na Shirika lisilokuwa la kiserikali la Dream Success Enterprises.

Kubenea ni nani? ni Mwanzilishi, Mhariri Mtendaji na Mkurugenzi wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited (HHPL), waliokuwa wakichapa gazeti la kufichua maovu la MwanaHALISI na baadaye serikali kulifungia kwa muda usiojulikana.

Kwa sasa baada ya gazeti hilo ambalo lillikuwa likiiumbua serikali kwa maovu yake anamiliki gazeti la mtandaoni la MwanahalisiOnline na MwanaHALISI Forum zenye kauli mbiu ‘Uhuru hauna mipaka’ .

Hapo awali Kubenea alisema kutoa dukuduku na kusema “Nimeamua kugombea jimbo la Ubungo ninaamini ni demokrasia na ni haki yangu kufanya hivyo kama mtanzania” huku akizungumza kwa kujiamini kwa kurejea kauli ya baba waTaifa, Mwl. Nyerere aliyesema “wananchi wana hitaji mabadiliko, wasipoyapata ndani CCM watayatafuta nje ya CCM”.

Kwa vile wananchi wameshindwa kupata mabadiliko ndani ya CCM , kubenea amesema ameamua kugombea nafasi hiyo kupitia tiketi ya Chadema, chama makini, iliaweze kuwa sehemuya Bunge ya kutunga sheria na kuisimamia serikali kwa maslahi mapana ya watanzania na ustawi wa nchi kwa ujumla.

Aidha, alisema kuwa kwa miaka mingi amekuwa akipambana na ukandamizaji wa serikali kwa njia ya kalamu kupitia magazeti yake, “nimekuwa nikifanya shughuli za Bunge nje ya Bunge” amesema sasa kuna umuhimu wa kuwa mbunge halisi na ninaamini nitakuwa mbunge mzuri na mwenye weledi kuitumikia nchi yangu kwani ninauzoefu mkubwa wa uendeshaji wa bunge lenyewe, siendi bungeni kujifunza kanuni za bunge kwani ninajua hata milango ya kutokea, Kubenea alisisitiza huku akijiamini.

 

error: Content is protected !!