Wednesday , 27 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kubenea ahoji vibali vya sukali kutoka nje
Habari za Siasa

Kubenea ahoji vibali vya sukali kutoka nje

Spread the love

MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema), ameihoji serikali na kutaka ieleze kama kitendo cha kutoa kibali cha viwanda vya sukari kuagiza sukari nje kutoka nje, siyo kuua kilimo cha zao la miwa ambacho wakulima wanategemea kuuza viwanda vya ndani. Anaripoti Danson Kaijage … (endelea).

Mbunge Ndanda, Cecil Mwambe (chadema) akimwakilisha Kubenea, ametoa hoja  hiyo leo tarehe 9 Septemba 2019 bungeni wakati wa kipindi cha maswali na majibu.

“Ni kweli kwamba bei ya bidhaa za viwanda kwa kiwango kikubwa zinatokana na gharama za uzalishaji. Je, kitendo cha kutoa kibali cha viwanda vya sukari kuagiza sukari nje kutoka nje kama siyo kuua kilimo cha zao la miwa, ambacho wakulima wanategemea kuuza viwanda vya ndani?” amehoji Kubenea.

Omary Mgumba, Naibu Waziri wa Kilimo amesema, serikali kupitia bodi ya sukari, imekuwa ikifanya tathimini ya mahitaji ya sukari nchini kwa mwaka kwa kuzingatia matumizi ya kawaida na matumizi ya viwandani.

Amesema, tathimini hiyo hufanyika sambamba na kujua uwezo wa viwanda vya kuzalisha sukari nchini, ambapo naksi kati ya uzalishaji na mahitaji ndio kiasi cha sukari inayohitajika kuagizwa kutoka nje ya nchi.

“Tathimini ya mahitaji ya sukari kwa miaka miwili iliyopita 2017/2018 na 2018/2019, ilibainika kuwepo na utengamano wa soko la ndani kwa bei ya upatikanaji wa sukari nchini.

“Aidha, utengamano huo ni matokeo ya maamuzi ya serikali ya kutumia mfumo wa kuwapa leseni wazalishaji wa ndani kuagiza sukari kutokana na mahitaji badala ya mfumo wa kutumia wafanyabiashara,” ameeleza Mgumba.

Mgumba amesema, katika kipindi cha uzalishaji miwa kwa wazalishaji wadogo umeongezeka kutoka tani 568,083 msimu wa 2017/2018 hadi tani 708,460  msimu wa 2018/2019.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!