March 3, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kubenea ahoji mabilioni ya makinikia

Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea akihoji jambo bungeni

Spread the love
Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea amemtaka Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi kulieleza Bunge majadiliano baina ya Serikali na Kampuni ya Madini ya Acacia kuhusu makinikia yamefikia wapi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Pia, amemtaka kuwaeleza Dola 190 bilioni zaidi ya Sh 424 trilioni zinazopaswa kulipwa na Acacia zitapatikanani lini.

Akichangia bajeti ya wizara ya nishati ya mwaka 2018/19 leo Juni 1, 2018, Kubenea amesema inasikitisha amesoma kitabu cha bajeti cha waziri na cha kamati hakuna walipozungumzia makinikia.

“Sisi tulitegemea Bunge letu tupewe taarifa ya kina kuhusu mazungumzo kati ya Serikali na Acacia. Tuelezwe Sh424 trilioni ambazo ni Dola bilioni 190 tungepata lakini Bajeti nzima imekuja haijazungumzia na ripoti ya waziri hakuna kokote,” amesema Kubenea

“Kwa kuwa mmoja wa wajumbe ni Profesa Kabudi atuambie makinikia imefikia wapi, mchanga uliozuiwa bandarini upo, utakuwapo hadi lini, mchanga unasafirisha? Kiwanda cha kuchenjua kitajengwa lini?” amehoji

Kubenea amesema fedha hizo Sh 424 trilioni zinapaswa kila Mtanzania apate matibabu, kuishi maisha mazuri kwa fedha hizo zinapatijkana lini?

 “Suala hili ni muhimu kuelezwa makinikia yako wapi. Mazungumzo yamefikia wapi, fedha zinapatikana lini ili tuipate. Tutajua kila wilaya, kata kitapata kituo cha afya, bajeti ya miaka kumi.”

“Fedha hizi ni nyingi sana na kama tumeibiwa, Serikali ijiangalie vizuri na ili kufikia malengo tusipige danadana tuimalishe Stamico itakayosimamia madini yetu,” amesema.

error: Content is protected !!