November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kubarua cha kwanza, kocha mpya Simba

Spread the love

 

KLABU ya soka ya Simba jana tarehe 6, Novemba 2021 ilimtangaza Pablo Franco Martin kuwa kocha mkuu wa kikosi hiko, ambaye amekuja kuchukua mikoba ya Didier Gomes aliyeamua kusitisha mkataba wake mara baada ya makubaliano ya pande zote mbili, huku akiwa na kibarua cha kuivusha timu hiyo hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho Barani Afrika. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kocha huyo ameingia mkataba wa miaka miwili, na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara na ataungana na kocha wa sasa Thierry Hitimana pamoja na Selaman Matola kwenye benchi lake.

Kibarua hiko kinakuwa kigumu kwa kocha huyo, kutokana na rekodi ya makocha waliopita kwenye klabu hiyo, walifanikiwa kuifikisha na kuivusha Simba kwenye hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa.

Msimu wa 2018/19 Patrick Aussems akiwa kocha wa Simba alifanikiwa kuipeleka tinu hiyo Robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, mara baada ya kukaa nje ya michuano hiyo kwa muda mrefu.

Msimu unaofuata kocha huyo alitimuliwa, huku ikiwa timu hiyo ilishindwa kufuzu kwenye makundi Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kutolewa na UD Songo ya msumbiji na mikoba yake kuchukukiwa na Sven Vandebroeck ambapo aliongoza Simba kwa mafanikio makubwa kwa kutwaa makombe mawili, Ligi Kuu na kombe la Shirikisho la Azam.

Pia kocha huyo aliweza kuirudisha timu hiyi kwenye ramani ya soka la kimataifa, mara baada ya kufuzu tena hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa, kisha akafunja mkataba wake na kutimkia nchini Morocco kwenye klbau ya FC Berkane.

Januari, 2021 Simba ilimtangaza Didier Gomes kama kocha mpya aliyekuja kuchukua mikoba ya Sven wakati Ligi ikiwa mzunguko wa pili na kuiongoza timu hiyo kwenye michezo ya makundi Ligi ya Mabingwa na kufanikiwa kumaliza kinara kwenye kundi A, mbele ya mabingwa watetezi wa michuano hiyo klabu ya Al Ahly.

Pablo anakuja kukinoa kikosi cha Simba huku mashabiki na uongozi wakiwa na shauku ya kufanya vizuri kwenye michuano ya kombe la Shirikisho ambayo walidondoshwa huko mara baada ya kutolewa kwenye mzunguko wa kwanza Ligi ya Mabingwa.

Kibarua cha kwanza kwa kocha huyu mpya kitakuwa dhidi ya Red Arrows kutoka Zambia, kwenye mcheo wa kombe la Shirikisho ambao Simba watanzia nyumbani.

Simba itafuzu hatua ya makundi, endapo itafanikiwa kuwafunga wazambia hao, kwenye michezo yote miwili.

Kikosi cha Simba kilikuwa chini ya Hitimana ambaye alikuwa kocha mkuu wa muda na kuingoza Simba kupata ushindi wa bao 1-0, kwenye mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu dhidi ya Namungi FC.

error: Content is protected !!