MWANASHERIA Mkuu wa Marekani, Jeff Sessions amejiuzulu wadhifa huo akitekeleza agizo la Rais Donald Trump, lililomtaka kuachia ngazi. Yanaripoti Mashirika ya Kimataifa …(endelea).
Trump alitoa agizo hilo jana tarehe 7 Novemba 2018, ikiwa ni masaa 24 baada ya chama chake cha Republican kupoteza udhibiti wake katika Bunge la Wawakilishi, kufuatia kuanguka katika uchaguzi wa kati kati ya muhula uliofanyika juzi Jumanne.
Katika barua yake ya kujiuzulu aliyoiwasilisha hapo jana, Sessions aliandika kwamba uamuzi wake wa kujiuzulu unatokana na agizo la Trump, lililomtaka kujiuzulu.
Kupitia akaunti yake ya Twitter, Trump alimpongeza Sessions kwa hatua yake ya kujiuzulu na utumishi wake wakati akiwa Mwanasheria Mkuu.
Katika hatua nyingine, Trump amemteua Matthew Whitaker kukaimu nafasi ya Mwanasheria Mkuu hadi pale atakapoteuliwa mtu kushikiliwa wadhifa huo.
Awali Trump alikuwa amekosana na Whitaker kutokana na kutofurahishwa kwake na hatua ya kujiondoa katika uchunguzi wa FBI kuhusu madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani 2016. Alidai kuwa Sessions alikuwa na msimamo dhaifu.
Leave a comment