April 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kuagwa Mkapa: Ndege ya mwakilishi Kenya, yashindwa kutua Tanzania

Profesa Palamagamba Kabudi

Spread the love

NDEGE iliyombeba mwakilishi wa Kenya, Samuel Poghisio aliyekuwa anakwenda Tanzania, kuhudhuria shughuli ya kitaifa ya kumuaga Hayati Benjamin Mkapa, Rais wa Awamu ya Tatu, imelazimika kurejea Kenya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa ya mwakilishi wa Uhuru Kenyatta, Rais wa Kenya kushindwa kufika kwenye shughuli hiyo leo Jumanne tarehe 28 Julai 2020, imetolewa na Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania.

Akizungumza kwenye shughuli hiyo leo Jumanne katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, Prof. Kabudi amesema, mpaka sasa (ilikuwa asubuhi) hawajapata taarifa kutokana na ndege hiyo kulazimika kurudi Kenya kabla ya kutua Tanzania kama ilivyokusudiwa.

Kwenye shughuli hiyo, Jenerali Alain Guillaume ambaye ni Waziri Mkuu wa Burundi, amefikisha salamu za rambirambi za rais wa taifa hilo Jenerali Evariste Ndayishimiye.

Samuel Poghisio

Amesema, Rais Ndayishimiye na Burundi yote wanawafariji Watanzania katika kipindi hiki kigumu, “muhimu ni tueendelea kumuombea Hayati Mkapa.”

Mwili wa Mpaka ulikuwa unaagwa kitaifa uwanjani hapo na kuongozwa na Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli.

Mkapa alifariki dunia Alhamisi tarehe 23 Julai 2020 saa 3:30 usiku kwa mshtuko wa moyo. Mwili wake, utazikwa kesho Jumatano kijijini kwake, Lupaso, Masasi Mkoa wa Mtwara.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

error: Content is protected !!