January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Korti yamwidhinisha Nkurunziza

Pierre Nkurunziza, Rais wa Burundi

Spread the love

PIERRE Nkurunziza-Rais wa Burundi, ameruhusiwa kuingia katika kinyang’anyiro cha urais kwa muhula wa tatu. Hii ni kwa mujibu wa uamuzi wa Mahakama ya Katiba ya Burundi chini ya jopo la majaji sita waliotia sahihi, huku mmoja wao akikataa.

Kwa mujibu wa Katiba ya Burundi, Rais anaruhusiwa kugombe kiti hicho kwa mihula miwili tu, hata hivyo swala hili lilijengewa hoja na mahakama ya katiba nakuonekana kuwa katiba haimbani Nkurunziza, kwani katika muhula wa kwanza mwaka 2005 alichaguliwa na Bunge la Seneti, hivyo kutohesababiwa kama ni muhula mmoja kwa mujibu wa Katiba.

Maamuzi haya ya mahakama hiyo yamepelekea maandamano mapya ya watu zaidi ya 500 katika mji mkuu wa Bujumbura.

Kabla ya maamuzi haya, Makamu wa Rais wa Mahakama ya Katiba, Sylvère Nimpagaritse ameripotiwa kuwa amekimbilia Rwanda kutokana na hofu ya kifo.

Nimpagaritse alisema kuwa wenzake walio wengi wanatambua kuwa muhula wa tatu ni kinyume cha katiba, hata hivyo walikuwa kwenye shinikizo na hivyo kuamua kubadilisha msimamo wao.

Uamuzi wa Chama tawala cha CNDD-FDD kupitisha jina la mgombea urais wa chama chao, uliotolewa tarehe 25 Aprili 2015, ulijibiwa kwa maandamano na fujo za wananchi,  maandamano makubwa kabisa kuwahi kutokea tangu usitishaji wa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2005.

Fujo hizo zilisababisha vifo vya watu 12 kwa mujibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu, hata hivyo kuna taarifa nyingine kuwa siku ya jumatatu kuna vifo vingine vitatu, huku watu 20,000 wakikimbia na kuomba hifadhi nchi jirani.

Jumatatu wiki hii, John Kerry- Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, akiwa Kenya alimtaka Nkurunziza kuachana na wazo lake la kugombea nafasi hiyo kwa mara ya tatu.

Umoja wa Afrika (AU), umeonyesha wasiwasi wake juu ya amani. Hata hivyo Aprili, Baraza la Usalama la AU liliwataka Warundi kuheshimu maamuzi ya Mahakama ya Katiba bila ya kujali mahakama hiyo itatoka na maamuzi gani.

Nkurunziza aliyekuwa kiongozi wa uasi na Mawenyekiti wa CNDD-FDD kabla hajawa Rais, amekuwa madarakani tangu mwaka 2005, alipochaguliwa na Bunge kufuatia makubaliano ya kusitisha vita vya wenyewe.

Mwaka 2010, alishinda uchaguzi wa Rais baada ya vyama vikuu vya upizani kususuia uchaguzi huo, kwa madai kuwa ulikuwa na hila.

error: Content is protected !!