May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Korea Kaskazini yatangaza karantini nchi nzima

Spread the love

 

KOREA KASKAZINI imetangaza amri ya kutotoka nje nchi nzima,baada ya kudhibitika kwa maambukizo ya kwanza ya Covid 19. Anaripoti Rhoda Kanuti kwa msaada wa Mashirika ya Kimataifa … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa na vyombo vya habari vya serikali, vimeripoti kuwa kuna mlipuko wa Omicron katika mji mkuu wa Pyongyang, lakini havikueleza idadi ya visa na maambukizi.KCNA ilisema kuwa ‘’tukio kubwa zaidi la dharura.’’

Hata hivyo Kiongozi Kim Jong -un alikuwa katika mazungumzo ya dharura ya kuandaa namna ya kukabiliana na mlipuko huo wa kitaifa.

Lakini wachunguzi wanaamini kuwa virusi hivyo, vilikuwepo nchini kwa muda mrefu.Korea Kaskazini hata hivyo haikuwachanja chanjo ya Covid 19 wananchi wake, baada ya kukataa ofaya chanjo ya Sinovac iliyotengenezwa China na AstraZeneca.

Taifa hilo limekuwa na lengo la kuzuia virusi kwa kufunga mipaka yake tangu kuanza kwa janga hilo, nakusababisha hali mbaya ya kiuchumi na uhaba wa chakula, kwani mtiririko wa bidhaa muhimu kwa nchi hiyo masikini ulipungua kwa kiasi kikubwa.

error: Content is protected !!