June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kongwa kupigwa msasa kusimamia bajeti

Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akitoka ndani ya nyumba ya mfano baada ya kuzindua nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma

Spread the love

WANANCHI  wa Mji mdogo wa Kibaigwa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, watajengewa uwezo wa kutafuta taarifa na kuzichambua ili waweze kufuatilia na kusimamia mipango ya bajeti na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi katika maeneo yao. Anaandika Dany Tibason, Kongwa …. (endelea). 

Mkurugenzi wa Asasi ya Afya ya Jamii Tanzania (AJAT), yenye makao yake katika Mji mdogo wa Kibaigwa, Abdallah Mbwasi amesema  mradi huo utatekelezwa kwa miaka mitatu unatarajia kukamilika Februari 2018.

“Lengo la mradi ni kuwajengea wananchi uwezo wa kutafuta taarifa na kuzichambua ili waweze kufuatilia na kusimamia mipango ya bajeti na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kijamii kiuchumi katika maeneo yao” amesema.

Amewataka  wananchi kuupokea mradi huo kwani utakuwa na manufaa kwao kwani kujengewa uwezo hupelekea kuamsha mambo mengi ambayo walikuwa hawayafahamu ikiwemo suala la ufuatiliaji wa bajeti. 

Amesema  elimu hiyo itawafanya wananchi wawe hata na uwezo wa kuhoji na kufuatilia taarifa za mapato na matumizi kwenye maeneo yao.

Amesema  mradi huo utatekelezwa kwa kushirikisha Asasi tatu ikiwemo Afya ya Jamii Tanzania ambayo itahusisha kata ya Kibaigwa na Ndurugumi, Asasi ya  AFNET itatekeleza mradi katika Kata ya Ugogoni na Mkoka na Asasi ya Umwema ambayo itatekeleza mradi katika Kata ya Mlali na Chamkoroma.

Aidha, amesema  mradi huo utawajengea uwezo wananchi  kudai uwajibikaji na utawala bora katika utoaji wa huduma bora za afya. 

Mbwasi amesema  mradi utaendesha semina juu ya ufuatiliaji na uwajibikaji jamii kwa viongozi wa seruikali ya mtaa, kamati za usimamizi na uendeshaji za zahanati za Kibaigwa na Ndurugumi.

Mradi huo umefadhiliwa na TACOSODE kwa msaada wa Watu wa Marekani.

error: Content is protected !!