July 31, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kongo yaikomalia UN ripoti ya siri

Spread the love

TUME ya uchaguzi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (CENI) imewataka Wataalamu wa Umoja wa Mataifa kutoa ripoti ya siri inayoonesha uwezekano wa kufanyika kwa Uchaguzi Umkuu nchini humo, anaandika Wolfram Mwalongo

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamesema, wanayo ripoti ya siri inayoonesha kwamba bila kubadili daftari la kupiga kura, kuna uwezekano DRC kufanya uchaguzi katika muda uliopangwa kwa mjibu wa katiba.

CENI imepinga taarifa za UN kwa kushindwa kutoa hadharani ripoti hiyo inayodaiwa kuonesha uwezekano wa kufanyika kwa uchaguzi licha ya umoja huo kudai umefanya hivyo kwa lengo la kutoingilia tume hiyo ya Kongo.

Hata hivyo mpaka sasa (CENI) haijaandikisha wapigakura ambapo inakadiriwa takribani miezi 16 itatumika kuandaa daftari hilo katika uchaguzi mkuu wa Aprili 2017 licha ya utawala wa Rais Joseph Kabila kutakiwa kukoma Dsemba 19 mwaka huu.

error: Content is protected !!