August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kongo wamtimua msemaji wa MONUSCO

Spread the love

SERIKALI ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imemtaka msemaji wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini humo (MONUSCO), Mathias Gilman kuondoka haraka iwezekanavyo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Serikali hiyo imesema msemaji huyo ametoa matamshi yasiyofaa yaliyochangia mvutano kati ya wananchi na MONUSCO.

Wiki iliyopita, watu 30 waliuawa wakati wa maandamano yaliyoibuka mashariki mwa nchi hiyo.

Miongoni mwa waliopoteza maisha ni walinda amani wa Umoja wa Mataifa na maofisa wa polisi.

Waandamanaji walilalamikia kile walichosema ni kushindwa kwa MONUSCO kuzuia mauaji yanayofanywa na makundi ya waasi.

Tarehe 31 Julai, 2022 watu watatu waliuawa baada ya walinda amani hao walipowafyatulia risasi katika kituo kimoja cha mpakani.

MONUSCO inakamilisha jukumu lake mwaka 2024 kwa mujibu wa mpango uliotangazwa mwaka jana, lakini serikali ya Kongo inataka iharakishe kuondoka kwake.

error: Content is protected !!