Thursday , 25 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Kongamano la miji ya Afrika lafunguliwa nchini Kenya
Kimataifa

Kongamano la miji ya Afrika lafunguliwa nchini Kenya

Raila Odinga
Spread the love

 

VIONGOZI magwiji wa soka na nyota wa Hollywood wanakutana leo,katika jiji la Kisumu kando ya Ziwa Victoria nchini Kenya,kwaajili ya Kongamano la Africities,kujadili suala la mabadiliko ya hali ya hewa na ukuaji wa miji. Anaripoti Rhoda Kanuti kwa msaada wa Mashirika ya Kimataifa … (endelea).

Mkutano huo utafanyika leo siku ya Jumanne tarehe 17 Mei 2022, katika jiji la Kisumu kando ya Ziwa Victoria, ulioandaliwa na Umoja wa Miji na Serikali za Mitaa, kila baada ya miaka mitatu ili kujadili changamoto za ukuaji wa miji na mabadiliko ya tabia nchi katika makazi ya watu barani Afrika.

Hata hivyo Rais Uhuru Kenyatta atafungua rasmi makaya 9 ya Africities, katika kongamano ambalo litaangazia jinsi majiji ya kati yenye wakazi kati ya 50,000,na milioni moja yanaweza kusaidia kukabiliana na masuala ya kisiasa kama vile mabadiliko ya hali ya hewa na uhaba wa nyumba.

Jiji la Kisumu, liko magharibi mwa Kenya ni jiji la kwanza la aina hiyo kuandaa mkutano huo,pia kitakachojadiliwa kwa muda wa siku zijazo nipamoja na majibu kwa janga la Covid 19 katika miji ya kati.

Pia miongoni mwa nyota wa kimataifa wanaohudhuria ni Pamoja na nyota wa soka Didier Drogba kutoka Ivory Coast na Mcameroon Samuel Etoo.

Aidha mwigizaji Lupita Nyongo ambaye ni balozi wa Africities, pia nanahudhuiria baba yake Lupita,Profesa Anyang Nyong’o ndiye gavana sasa wa jimbo la Kisumu ,ambaye ndio mwenyeji wa mkutano huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!