Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Makala & Uchambuzi Kondomu zinavyotumika kufukuza Tembo
Makala & Uchambuzi

Kondomu zinavyotumika kufukuza Tembo

Spread the love

MIKUMI ni miongoni mwa hifadhi za Taifa, inashika nafasi ya 9 kwa ukubwa kati ya hifadhi 22 zinazosimamiwa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), ilianzishwa mwaka 1964.

Ni hifadhi nzuri kwa utalii wa safari. Wanyama wote wakubwa wanapatika wakiwamo Tembo, Nyati, Simba na Chui isipokuwa Kifaru ambaye alipotea kwa sababu ya ujangili.

Namna ya kutengeneza bomu la pilipili.

Imezungukwa na wananchi ambao wengi wao wanajishughulisha na kilimo. Hata hivyo, shughuli za kilimo zinatatizwa na wanyama hususan Tembo ambao wanavamia mashamba na kuharibu mazao.

Katika kukabiliana na wanyama hao, kuna mbinu mbalimbali zinatumika ikiwamo kutumia uzio wa pilipili wenye mchanganyiko wa tumbaku na mafuta ya kondoo, tofali za pilipili, tochi zenye mwanga mkali, honi mfano wa vuvuzela, fataki kubwa na uzio wa mizinga ya nyuki.

Ofisa Mwandamizi ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Utalii Hifadhi ya Taifa Mikumi, Herman Mtei anasema kwa kutambua kuwa wananchi ndio wahifadhi namba moja wamekuwa wakiwashirikisha katika shughuli mbalimbali za uhifadhi.

Anasema ili kuwaweka karibu zaidi wananchi na uhifadhi, TANAPA imeanzisha mradi wa REGROW kwa kufadhili vijiji na vikundi mbalimbali, ambapo kupitia hiyo miradi jamii inaona umuhimu wa uwepo wa uhifadhi.

“Tumetoa ufadhili wa masomo kuanzia ngazi ya cheti hadi shahada ya kwanza, pia mafunzo ya kufuga nyuki, wakulima wadogo wanapatiwa elimu ya namna ya kufunga mawigo kwenye mashamba ili yasivamiwe na Tembo,” anasema Mtei na kuongeza kuwa;

“Kutokana na watu kuwa karibu na hifadhi hii, baadhi yao walikuwa wakijishughulisha na ujangili kwa kuwatega Tembo ili kuwang’oa meno, lakini kupitia REGROW Kikundi cha Mawigo kimekuwa kikijishughulisha na ulinzi wa Tembo na kulinda mazao yasiharibiwe na wanyamapori hao.”

Mhifadhi Wanyamapori Tarafa ya Mikumi, Makene Ngoroma ambaye amepata mafunzo kupitia mradi wa REGROW, katika kuhakikisha kuwa mfumo wa kilimo unaboreka, lakini pia wakulima wanalinda mazingira na kuishi kwa amani na wanyamapori amebuni mbinu mpya inayosaidia kukabiliana na uharibifu wa mazao.

“Katika jamii zimekuwepo mbinu ambazo kimsingi zimezoeleka kwa Tembo, ukiwemo mwanga wa tochi, ila kwa sasa tumeamua kuziboresha kwa kuja na mbinu ya utumiaji mabomu ya pilipili,” anaeleza Ngoroma.

Anasema kuwa mbinu hiyo mpya ya kufukuza Tembo kuvamia mashamba ni rafiki na shirikishi, na kuwa wamekuja na mbinu hiyo chini ya mpango mkakati wa kupunguza migongano baina ya binadamu na wanyamapori kuzunguka Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.

Mbinu hiyo mpya ya kuwafukuza wanyamapori wasiharibu mashamba, ni kuwa wanatumia kondomu za kiume zinazowekwa mchanga na unga wa pilipili (Chili powder).

“Jamii yetu ipo pembezoni mwa mbuga za wanyama, wakati mwingine wanyamapori hususan Tembo wanakuja katika mashamba na hata kuharibu mazao kitendo ambacho kinamuumiza mkulima,” anasema.

Mhifadhi huyo anabainisha namna bomu la pilipili linavyoandaliwa. Anasema ili kutengeneza bomu hilo unachukua kondomu kavu, fataki, unga wa pilipili na mchanga na kuweka vijiko vinne vya unga wa pilipili halafu unafunga fataki vizuri kwenye mdomo wa kondomu baada ya kuweka mchanga.

Anasema kuwa pindi unapoona Tembo wamevamia shamba ndipo unawasha utambi wa fataki huku ukiwa umekadiria umbali mpaka utambi utakapomalizika kuwaka ndipo unarusha upande alipo Tembo. Baada ya fataki kulipuka kondomu itapasuka na pilipili itasambaa angani na kumghasi mnyama huyo na kulazimika kurudi alipotoka (hifadhini).

“Tumekuja na mbinu hii kwani inafanya kazi mara mbili; mlio wa fataki kama kelele na pilipili. Hivyo, niwaombe wakulima wanaosumbuliwa na Tembo walime pilipili kama zao la biashara na zao la kuzuia wanyamapori hususan Tembo,” anatoa mwito na kuongeza;

“Pia wakulima walime mashamba yao mbali na njia za Tembo wasilime kwenye shoroba za Tembo na watumie mbinu za uzio wa pilipili, bomu la pilipili na tofali la pilipili.”

Kwa kutambua umuhimu wa uhifadhi hivi karibuni, Chama cha Waandishi wa Mazingira (JET) na Internews waliandaa mafunzo kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ili kuwajengea uwezo ambao utawasaidia kupaza sauti ili jamii itambue umuhimu wa kuhifadhi mazingira zikiwemo hifadhi za Taifa.

Kimsingi wahariri hao baada ya mafunzo walikutana na vikundi vinavyojishughulisha na uhifadhi wa mazingira katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi kwa kufadhiliwa na TANAPA na kujifunza shughuli za uhifadhi zinazofanywa na vikundi hivyo kwa faida ya Watanzania wote.

Shughuli nyingine zinazofanywa na vikundi hivyo takriban 15 ni kuondoa taka ndani ya hifadhi, ufugaji kuku, nyuki, ulinzi wa wanyapori na shughuli nyingine. Na kwa kuwa mazingira ni uhai; tunapaswa tuyalinde na tuyatunze ili tuishi. Makala hii imeandaliwa na Anicetus Mwesa…(endelea).

1 Comment

  • Wapambania haki za Binadamu wamebuni Mbinu za Mwanamke kupata SIFA ZINAZOSTAHIZI KWA KUMWEKEA VIKWAZON VYA KILA MTU ANATAKIWA KUMUONA MWANAE ALIYEMZAA (MZEE/kabila ANATAKA URAISI KULE ULIKOENDA KUONA)…

    KAMA UNA MATOTO WA KIKE UNAJUA FURSA ULIONAYO KAMA MZAZI

    KAMA UNA MTOTO WA KIUME UNAJUA FURSA ULIYONAYO USIMSAHAU BASH YUPO KULE

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Miaka 28 watumishi UDSM yaliwa na nzige, madumadu

Spread the loveGEORGE Francis anasikitika; anatembea akiwa na mawazo mengi, hajui la...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nimekumbuka Samia wa miaka 3 iliyopita

Spread the loveWAKATI naandaa makala ya safu hii wiki hii, nimejikuta nakumbuka...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Hakuna fedha za Rais

Spread the loveKUNA mambo machache mazuri ya kujifunza kutoka kwa Margaret Thatcher,...

error: Content is protected !!