Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Kondoa wanufaika na Bil 1 za Tasaf
Habari Mchanganyiko

Kondoa wanufaika na Bil 1 za Tasaf

Maofisa wa Tasaf walipotembelea moja ya kaya maskini
Spread the love

ZAIDI ya Sh. bilioni moja zimetumika kuwalipwa walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini unaofadhiriwa na mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF kwa kipindi cha mwezi Septemba hadi Disemba 2016 walioshiriki katika kutekeleza miradi ya ajira za muda na kujiongezea kipato, anaandika Dany Tibason.

Hayo yalibainishwa juzi na Mhasibu wa Tasaf wilaya ya Kondoa, Bezarel Buremo wakati alipokuwa akizungumzia utekelzaji wa miradi ya ajira za muda (PWP) kwa walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini nchini.

Buremo amesema kuwa katika utekelezaji wa miradi hiyo ya ajira za muda kwa walengwa ambapo uibuaji pamoja na upangaji ufanywa na wananchi wenyewe kwa njia shirikishi na wanapohudhuria hulipwa ujira wa kujikimu kwa familia zao kwa siku kiasi cha Sh. 2,300 kwa kipimo maalumu kisicho zidi masaa mawili ya kazi.

Alifafanua kuwa miradi ya ajira za muda imetekelezwa katika wilaya ya Kondoa kwa vijiji 84 katika kipindhi cha mwezi Septemba hadi Disemba mwaka 2016 na kiasi hicho cha fedha kutumika kwajili ya malipo ya ujira.

“Kiasi cha zaidi ya Sh. bilioni 1.3 kimelipwa kwa walengwa walioshiriki katika utekelezaji wa miradi ya ajira ya muda na kuongeza kipato kwa kaya 10,391 kutoka vijiji 84 vya wilaya hii ya kondoa,” amesema Buremo.

Naye Mratibu wa mpago huo wilayani hapo, Donald Jiday amesema kuwa miradi ya utekezaji ajira ya muda kwa walengwa wa Tasaf ilikuwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya huduma za jamii kama vile maji, ujenzi wa skimu za umwagiliaji, masoko ya mazao ya wakulima na wafugaji, ujenzi wa madarasa, hosteli za wanafunzi, zahanati pamoja na nyumba za watumishi.

Amesema kuwa katika miradi ya skimu za umwagiliaji walengwa walioshiriki walipwa ujira kama sehemu ya kutambua mchango wa nguvu zao lakini pia miradi hiyo wataitumia katika kuendeleza familia zao kujikwamua kiuchumi kwa kuendesha shughuli mbalimbali za uzalishaji mali.

“Walengwa hawa pamoja na kuwapatia kiasi cha fedha wakati wa utekekezaji wa miradi hii ya ajira ya muda lakini pia mradi kama ile ya uchimbaji wa mabwawa kwa ajili ya kuvuna maji ya mvua watayatumia kipindi chote ambacho kitakuwa hakina mvua ili kuweza kuendesha kilimo cha umwagiliaji cha mazao na mbogamboga ili kuweza kukabiliana na umaskini katika kaya zao,” amesema Jiday.

Mmoja wa walengwa wilayani hapo, Fatma Iddy amesema kuwa mpango huo umewawezesha kuweza kujikimu kutoka na kupata kiasi cha fedha ambacho wameweza kukitumia katika kuanzisha miradi kama vile ufugaji kuku pamoja na mbuzi ambayo inawawezesha kujikiku wao pamoja na familia zao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Watendaji Kata, Mitaa watakaoshindwa kusimamia usafi kukiona

Spread the love  WATENDAJI wa kata, mitaa na vitongoji na maofisa afya...

Habari Mchanganyiko

Mtia nia urais TLS kukata rufaa kupinga kuenguliwa

Spread the love  MTIA nia ya kugombea Urais wa Chama cha Mawakili...

Habari Mchanganyiko

NBC yazindua kampeni ya mkeka wa ushindi na ATM zake

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza uzinduzi wa kampeni...

Habari Mchanganyiko

Uholanzi wampongeza Rais Samia kuimarisha vyombo vya habari, demokrasia

Spread the love  UBALOZI wa Uholanzi nchini Tanzania, umempongeza Rais Samia Suluhu...

error: Content is protected !!